KWA NINI CARRICK ANAONDOKA?
Ni jambo la kushangaza kwa watu wengi,si tu kwa mashabiki wa United bali hata kwa wapinzani baada ya Carrick kuamua kung'atuka baada ya kumaliza muda wake mpito baada ya kufukuzwa kwa kocha Ole Gunnar Solskjaer.
Kabla ya kustaafu Mourinho ambae alikua ni kocha wa Man United aliwahi kusema
"nina wachezaji ambao wanaonyesha nia ya kuwa makocha baadae,na nawajua kutokana na maswali yao,Carrick ni mmoja wao"
Baada ya kustaafu tu Mourinho akampa ofa Carrick ya kuwa kwenye benchi la ufundi kama third assistant coach.
Hata baada ya Mourinho kuondoka haikumfanya Carrick kukata tamaa na kuamua kujipendekeza kwa Ole ambae kwa wakati huo alikua ni kocha wa mpito na kupata tena nafasi ya kuwa kocha msaidizi (assintant Coach).
Usichokijua ni kwamba Carrick muda wote aliokua United amekua akiwasiliana na Jose Mourinho na kuchukua hints mbalimbali kutoka kwake.👌
Maamuzi ya Carrick ni kujifua zaidi kupitia vilabu vengine na kupata uzoefu zaidi kwani anaamini bado hakuwa na nafasi ya kuiongoza timu ambayo yeye mwenyewe anaamini ni kubwa sana na inahitaji uzoefu zaidi wa mapambano ni vilabu vikubwa kwenye ligi na barani Ulaya.
Sitoshangaa kumuona Carrick akipumzika kwa miezi kadhaa na kujiunga kilabu chochote nchini England au Scotland.
0 Comments