club ya Simba Sc kutoka Tanzani ni moja kati ya vilabu ambavyo VIPO kwenye michuano ya kimataifa ya vilabu bingwa africa, Simba ilipata nafasi ya kuendelea mbele baada ya wapinzani wao ambao ndio walikuwa ndio mabingwa msimu uliopita kushindwa na kushuka kuelekea kombe la shirikisho.
Simba iliingia robo fainali kwakishindo kwakuifunga Horoya Fc ya kutoka Guinea huku ikiwa bado ina mechi moja mkononi ambayo ni ya marudiano na Raja Casablanca baada ya matokeo hayo viongozi wa Simba walipata nafasi ya kuongea kidogo kuhusu hilo
"Tunamshukuru mungu mpaka kufika katika hatua hii, ambayo kwa bahati nzuri tuna uzoefu nayo karibu miaka minne mfululizo tunaifikia, lakini bado tunaendelea kupambania nafasi ya huu zaidi kwani lengo na nguvu zetu kwenye haya mashindano, ni kutaka kuchukua ubingwa au hata tufikie nusu fainali kwani ndio nafasi ambayo huwa tunaiwaza lila kukicha... ili kufika ubingwa ni lazima tuhakikishe tunafika hata nusu fainali ili tuwe na mipango mikubwa ya kupambana kwa damu na jasho ili tufikie fainali, tumejipanga vizuri..."
"Pamoja na kuwa wanatuambia tuna kikosi kibaya mara tuna migogoro na maneno mengi tuu ambayo wanazungumza watu, ni maneno ambayo tangu Simba inaanzishwa yalikuwepo na unaweza kuta yalikuwepo maneno makubwa zaidi ya haya, lkin tunapambana ili tuwaoneshe kwamba maneno yao wanayongea kuusu Sisi ni maneno tuu ambayo kwetu hapana madhara yoyote."
0 Comments