MFALME wa miondoko ya Takeu, Hamis Ramadhan ‘H Baba’ amefunguka kuwa
gazeti (la Global Publishers) lilikuwa kigezo kikuu cha yeye kumtia
mikononi, mkewe muigizaji, Flora Mvungi.
Akizungumza na Global TV Online
kwenye kupitia Kipindi cha Mtu Kati kinachorushwa hewani leo, H Baba
aliweka plain kuwa alisota kwa takriban miaka miwili kumfukuzia Flora
lakini alikuwa akichomoa kwa kigezo kuwa ana mtu wake.
Alisema wakati akiendelea kuimbisha, baadaye moja kati ya magazeti ya Global yakaripoti kwamba mtu wake huyo ana mke na watoto wawili.
“Daah! Nawashukuru sana Global, Flora alikuwa hanielewi, lilipotoka hilo gazeti nikampigia na kwenda kumuonesha kuwa huyo mwanaume aliyeamini ndiyo mpenzi wake kumbe ana mke na watoto wawili,” alisema H Baba.
Flora na H. Baba waliooana mwaka jana, tayari wamebarikiwa mtoto mmoja mwenye umri wa miezi mitano.
WASIKILIZE H BABA NA MKEWE FLORA MVUNGI WALIPOLONGA NA GLOBAL TV ONLINE NDANI YA MTU KATI
Alisema wakati akiendelea kuimbisha, baadaye moja kati ya magazeti ya Global yakaripoti kwamba mtu wake huyo ana mke na watoto wawili.
“Daah! Nawashukuru sana Global, Flora alikuwa hanielewi, lilipotoka hilo gazeti nikampigia na kwenda kumuonesha kuwa huyo mwanaume aliyeamini ndiyo mpenzi wake kumbe ana mke na watoto wawili,” alisema H Baba.
Flora na H. Baba waliooana mwaka jana, tayari wamebarikiwa mtoto mmoja mwenye umri wa miezi mitano.
Tags
Michezo na burudani