Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

H BABA: GAZETI LILINIPA MKE





GLOBAL TV ONLINE; MTU KATI NA H BABA, FLORA MVUNGI

H Baba na mkewe Flora Mvungi wakihojiwa ndani ya Global TV Online.

MFALME wa miondoko ya Takeu, Hamis Ramadhan ‘H Baba’ amefunguka kuwa gazeti (la Global Publishers) lilikuwa kigezo kikuu cha yeye kumtia mikononi, mkewe muigizaji, Flora Mvungi.

WASIKILIZE H BABA NA MKEWE FLORA MVUNGI WALIPOLONGA NA GLOBAL TV ONLINE NDANI YA MTU KATI
Akizungumza na Global TV Online kwenye kupitia Kipindi cha Mtu Kati kinachorushwa hewani leo, H Baba aliweka plain kuwa alisota kwa takriban miaka miwili kumfukuzia Flora lakini alikuwa akichomoa kwa kigezo kuwa ana mtu wake.
Alisema wakati akiendelea kuimbisha, baadaye moja kati ya magazeti ya Global yakaripoti kwamba mtu wake huyo ana mke na watoto wawili.
“Daah! Nawashukuru sana Global, Flora alikuwa hanielewi, lilipotoka hilo gazeti nikampigia na kwenda kumuonesha kuwa huyo mwanaume aliyeamini ndiyo mpenzi wake kumbe ana mke na watoto wawili,” alisema H Baba.
Flora na H. Baba waliooana mwaka jana, tayari wamebarikiwa mtoto mmoja mwenye umri wa miezi mitano.

Post a Comment

0 Comments