Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Sifa Kuu Tano Za Mwanamke Ambazo Mwanaume Kamili Anapenda Kuziona Ama Kuzikuta Kwa Mwenza Wake.





1. Mwanamke anapaswa kuwa na maisha yake na sio maisha ya kuiga. Wapo wanawake ambao hupenda kuiga kile kinachofanywa na wanawake wenzake na kudhani hivyo ndivyo anavyopaswa kuwa.
mwanamke mwenye tabia hiyo huwa hana mvuto kwa mwanaume kwani atakuwa ni mwana mke fake.

2. Mwanamke anapaswa kuwa mtiifu na mwenye heshima na pia mwenye busara. Mwanamke hapaswi kuwa na kiburi na kutaka kuota mapembe ndani ya mahusiano. Heshima na utiifu haimaanishi kuwa tayari kunyanyaswa, hapana. Mwanamke anapaswa ampe mpenzi wake ama mumewe heshima inayotakiwa kama kichwa cha mahusiano yenu.

3. Mwanamke anapaswa kuwa na uwezo wa kujitegemea. Hapa utata kidogo, wapo wale wanaoamini kuwa mwanamke anapaswa kutegemea kila kitu toka kwa mwenza wake. lakini ukweli ni kwamba wanaume wengi wanapenda kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye anaweza kusimama kwa miguu yake na kujitegemea pia.

4.Mwanamke lazima awe anajiamini. Naam, hapa haimaanishi kuwa anatakiwa kuwa kiburi na mbishi, hapana. Isipokuwa mwanamke anapaswa aonyeshe kujiamini kwa kile anacosema na anachotenda. Kujiamini kunamfanya mwanaume ajue kuwa ana mpenzi ama mke ambaye anaweza kukabiliana na mikwaruzo mbalimbali inayohitaji hoja na utetezi.

5. Mwisho, mwanamke anapaswa kuwa na mvuto. Hapa haimaanishi kuwa mrembo saaaana, hapana. Ina maana kuwa mwanamke anapaswa kuwa nadhifu kila wakati ili kumfanya mwanaume apende kuwa nawe na avutiwe kuwa nawe wakati wote.

Sifa hizi tano akiwa nazo mwanamke, basi atambue fika kuwa Mwanaume atavutiwa nawe na uhusiano wenu unaweza kudumu na kudumu na kudumu. Unaweza kuongeza sifa nyingine hapa chini.
Source Jm

Sifa Zingine Ziko Hapa
Tabia ambazo ni za msingi sana kwa mwanamke yeyote anayefaa kuwa mke ni kama vile:-
Ajiheshimu:- hii ni sifa namba moja kwa mwanamke yeyote yule, heshima hii ni pana sana, kwamba aheshimu nafasi yake kama mwanamke kiasi kwamba awe tayari kumfurahisha mumewe zaid kuliko mwanaume mwingine yyte yule. pia aweze kuheshimu mwili wake, kwa mavazi ya heshima, mwonekano wa heshima na hata mwenendo tu wa heshima.
Siku hizi utakuta mdada anapita tu unaskia huyu ni wa hit and run tu hana future at first site mtu aliona nini manake pengine hamjui huyu dada ila aliangalia mwonekano tu japo pia waweza kudanganya but mara nyingi husema kweli.

Awe msafi:- hapa tunaongelea usafi wa mazingira yote, siyo wa mwili tu. Jamani tena hapa huwa usafi hauangalii wakati au aweo. Kuna mwanamke mwingine unamwona mchafu tu hata gari analoendesha tu chafu toka ndani hadi nje, sasa hapo jiulize huko nyumbani vipi? pia mwili siyo minywele wigi wiki nne hadi linanuka, miguu makegeta na vumbi hadi kwenye ugoko lol. hii ni mbaya sana. Mwingine hata kula tu ni kwa uchafu anamwaga meza yote akishika glasi ya juisi lol lazima ajimwagie kwenye nguo na wala hajali mwingine hata kiti tu cha kukalia hakagui anajikalisha tu kama pasi kujali,hii siyo tabia ya kike kabisa.

Ajue thamani yake kama mke au mchumba wa mtu:- hili ni gumu sana kwa baadhi ya wakina dada. utakuta she does’t know how wealth she is as a woman. ukishajua thamani yako kama mama utajua unamzigo kiasi gani wa kulea so utaitafuta hekima zaid na busara kuliko mzaha. Tena utajua nini wajibu wako kwa familia yako.

Awe mkarimu:- ukarimu hauna mipaka ni kwa wale wa ndani na hata wale wa nje ya nyumba yako. Mwanamke mkarimu huwa habagui, wala haumii nafsi anapotoa kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake hulisha, kuvesha kunywesha na kufariji wote pasi kunung’unika. silaha hii ikitumiwa vizuri huondoa umaskini, kutokufanikiwa, mikosi, na balaa. Huongeza ustawi wa familia, kipato,neema na mafanikio. hata siku moja huwez kosa ridhiki kwa kulisha watu wa nyumbani mwako, au kumkarimu mgeni.

Awe na upendo wa kweli si tu kwa mumewe bali kwa wote aliopewa na Mungu wawe wake:- iwe ni ngugu wa mume, au ndugu zake iwe ni watumisha wake majirani na hata wageni. Hii ni silaha ambayo huwa ikitumiwa vizuri pasi unafiki hubomoa misingi yote ya chuki, mafarakano, mikosi,balaa na yote yakufanana na hayo. huongeza umoja wa kifamilia,mshikamano, furaha na amani.
usafi wa mwili na mazingira-Yaani hili ni jambo la msingi sana, kwa mama yyte yule ambaye anaipenda familia yake. silaha hii hukinga familia dhidi ya magonjwa na pia hudumisha afya ya familia. ikitumiwa vizuri hupunguza matumizi ya fedha kwa kiasi kikubwa sana.

Awe na nidhamu katika matumizi ya hela:- mwanamke mzuri hayuko extra vagant na matumizi ya hela anajua kupanga resonable budget, na anajua resource utilization. hawez akatumia vitu hovyo pasi kujali kama vinaisha au vinaharibika. huwa ana mipango madhubuti juu ya vyombo vyake vya ndani, vyakula fedha na hata nishati kama gesi na umeme na hata maji.

Awe ni mcha mungu: this is prime quality kwa mwanamke yoyote mwenye familia. kwani lazima anajue kuwa maadili na misingi ya familia yake inajengwa ndani ya mungu anayemwabudu. atawashawish watu wa nyumbani mwake kusali, na tawalea wanae katika njia nzuri.

Ishu ya kujua kufanya mapenzi ni secondary characteristics kwani huwa tunategemea aanze kufanya tendo la ndoa baada ya ndoa so kujua ama kutokujua watajifunza wao wenyewe wawili kwa jinsi na namna wapendavyo wao wenyewe. huwezi kuiga haya ingawa kuna common aspects but variation ni kubwa sana wapo ambao hawapendi vibrations but wapo wanaozipenda kama ndugu yangu Kongosho so watabuni aina yao wenyewe ya love making.

All in all mwanamke aanawajibu wa kutambua kuwa yeye ndiye muumbaji ndani ya nyumba kwakua ndiye mwenye mikono inayofinyanga, anapaswa ajue hata mende aliyeko ndani mwake ni kwasababu yake na yeye ndiye anayemlisha so she has to be very smart in whatever she is doing, tena asiwe mvivu, wala msengenyaji wala asiyejua wajibu wake wa familia.

Post a Comment

0 Comments