Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

DIAMOND SASA MATATANI KWA KUHUSISHWA NA UUZAJI WA MADAWA CHINA, SOMA KILICHOMKUTA HAPA

STAA wa muziki wa bongo fleva nchini, Abdul Nassib "Diamond" ametakiwa kutokanyaga kabisa nchini China na kwamba akitokeza pua yake nchini humo asahau kabisa kurudi uraiani...

Hiyo inafuatia kijana mmoja mtanzania kukamatwa wiki iliyopita uwanja wa ndege wa Macau China na kudai kuwa yeye ni mcheza shoo wa mwanamuziki Diamond kutoka Tanzania....

Habari kutoka Macau China zinadai kuwa kijana huyo aliyejulikana kwa jina moja la Manyota alikamatwa akiwa kwenye harakati za kuingiza mzigo huo wa dawa za kulevya kwa kupitia uwanja wa ndege wa Macau....

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, inaarifiwa kuwa Manyota alikamatwa Alhamisi ya wiki iliyopita katika uwanja uleule aliokamatwa mtanzania mwingine Jackline Patrick, anayesotea rumande mpaka hii leo huko huko Macau China.....

Kijana mmoja wa kitanzania anayefanya shughuli zake huko China amedai kuwa Manyota alikamatwa na maofisa wa usalama wa uwanja wa ndege na katika utetezi wake alidai kuwa yeye ni mwanamuziki toka Afrika Mashariki...

Mtanzania huyo aliendelea kudai kuwa, Manyota baada ya kukamatwa alianza kubabaika kwa kujifanya mwanamuziki na baadae akadai kuwa yeye ni mcheza shoo wa mwanamuziki Diamond kutoka Tanzania....

"Alijifanya yeye ni mwanamuziki, baadae akabadilika na kudai yeye ni mcheza shoo wa mwanamuziki Diamond kutoka Tanzania na kwamba ndani ya ule mzigo alikuwa hajui kuna nini zaidi ya kuombwa na jamaa zake wa Dar awapelekee nchini China"...Alisema mtanzania huyo

Inasemekana kuwa, ili kujiridhisha, maofisa hao wa usalama wa uwanja wa ndege walimtaka kijana huyo aoneshe moja ya kazi zake na yeye akaishia kuwaonesha moja ya video za Diamond kupitia mtandaoni na kumuonesha mmoja wa wacheza shoo wa mwanamuziki huyo kuwa ndo yeye Manyota...

Inasemekana kuwa, pamoja na utetezi wake huo ambao unaweza kumuingiza matatani Diamond,maofisa hao wa usalama walishndwa kumuelewa na kumtupa ndani.....

Mtanzania huyo alihitimisha kwa kudai kuwa, kutokana na mazingira yalivyo,ni vyema mwanamuzi Diamond akawa makini sana kama atakuwa na safari za kwenda China kwani kwa namna moja ama nyingine jina lake limewekwa kwenye orodha ya majina machafu na wanaweza kumkamata kwa lengo la kuujua ukweli....

Post a Comment

0 Comments