Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

sakata la Wema na Kajala: Martin Kadinda afunguka




Martin Kadinda ambae ni meneja wa Wema Sepetu leo kupitia mitandao ya kijamii
ameamua kufunguka juu ya kile kinachoendelea kati ya Wema Sepetu na Kajala......
Nanukuu
Good morning all of You.... I just woke up Like "Hasiraless" kwakuwa hili vugu vugu la kutokuwa na maelewano mazuri kati ya Wema sepetu (myclient) na kajala limekuzwa katika social networks basi na mimi naomba nitoe taarifa kutoka kwetu endless fame.... katika urafiki kuna mengi yanajitokeza na endapo kutakuwa na hitilafu sehemu basi ni muhimu kupeana nafasi ili kila mtu aweze kujirekebisha na mwisho wa siku maisha yaendelee hilo ndo lililotokea baina ya hawa wawili... lakini katika kipindi hicho cha so called mapumziko kuna mambo mengi yamejitokeza.... yapo ya kweli na yapo yaliyotengenezwa na baadhi ya watu.. kuna media coverage juu ya hawa wawili na wema sikumpa nafasi ya kuzungumza na chombo chochote cha habari kwakuwa nilijua litakuzwa zaidi... ila tulipoona shutuma zinazidi kuja upande wake akafanya interview na gazeti moja na kuelezea upande wake na mwisho alisema hana tatizo na kajala sema tu Kwa sasa anahitaji space...... tukawa tumefunga mjadala huo...... endless fame(wema sepetu) haijawahi kutamka lolote swala la mahusiano ya kajala na mtu yoyote.... endless fame haijawahi kudoubt urafiki wa kajala na any of her friends because tunaamini yale ni maisha yake binafsi na hayahusiani na kampuni ya wema au wema mwenyewe, kusaidiana katika matatizo haimaanishi tunammiliki... hapana hapana... Hili linaloendelea sasa sisi pia tumelisikia na kuliona kwenye social networks kama watu wengine wanavyoona. Tunaumizwa na blogs na magazeti yanapoandika stori kama vile wanaushahidi kutoka endless fame au Kwa mtu wa karibu na wema. Team wema wote waliopo insta sijawahi kuona hata mmoja kati yao hivyo hakuna anayewatuma wala kuwashinikiza ila wao wanafanya kile kinachowapendeza and hatuwezi kuwakataza kwasababu ni maisha yao binafsi na ni mapenzi yao ya dhati Kwa wema... Poleni Kwa wote mnaoumizwa na haya yanayoendelea ila nadhani tukazane na kazi zetu na maisha yetu maana haya ya instagram tuwaache huku huku ukiyasikiliza utashindwa kumwamini mama yako mzazi. Tusiishi fake life in instagram while in really hatuna hata hela ya chumvi

Post a Comment

0 Comments