humph the GREAT
Azam FC imeamua
kuachana na kipa wake mkongwe Ivo Mapunda waliyemsajili msimu uliopita
kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake, huku wakifanya mchakato wa
kumsajili kipa mwingine.
Ivo ambaye ni kipa mkongwe
alitua Azam FC msimu uliopita akitokea Simba baada ya kushindwa
kumsajili katika dakika za mwisho ambapo wanalambalamba hao waliamua
kumpa mkataba wa mwaka mmoja.
Katibu Mkuu wa Azam FC,
Idrisa Nassor amesema kuwa, hawataendelea na Ivo msimu ujao wa ligi kuu
na kwa sasa wanafanya mchakato wa kusajili kipa mwingine atakayeziba
nafasi yake.
“Hatutarajii kuendelea na
Ivo msimu ujao wa ligi kuu na badala yake nafasi yake itachukuliwa na
kipa mwingine ambaye tunafanya mchakato wa kumsajili ili kuziba nafasi
hiyo.
“Kwa sasa amebakiza miezi
mitatu ili kukamilisha mkataba wake na Azam aliosaini mwaka mmoja msimu
uliopita na baada ya hapo tutaangana alisema bosi huy
Tags
Michezo na burudani