humphrey the GREAT
Kufuatia kupigwa mwereka kwenye
Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida,
staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amekiri kwamba
kilichomponza katika kinyang’anyiro hicho ni skendo za ngono hivyo kwa
sasa atakuwa makini ili asichafuke.
MAPOKEZI
A photo posted by wemasepetu (@wemasepetu) on
Akizungumza na gazeti hili baada ya
kupokelewa kishujaa na kuacha historia jijini Dar aliporejea kutoka
Singida wikiendi iliyopita, Wema alisema mashabiki wake hawatamsikia
tena na skendo hizo huku akiahidi kuibuka na bonge la ‘surprise’.
UMAKINI
“Shukurani zangu zipo palepale kwa mashabiki wote wanaonisapoti.
“Ninachowaahidi kwa sasa ni kuwa makini
na skendo lakini pia kuna kitu cha kushtua nitafanya hivi karibuni
ambacho kitaibua surprise (mshtuko) nzito kwa mashabiki wangu,” alisema
Wema.
TEAM WEMA
Katika mapokezi hayo ambayo gazeti hili
lilikuwa mstari wa mbele, makundi ya mashabiki wake na yale ya Team Wema
yalipeana taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa kipenzi chao, Wema
angefika Dar, Jumapili iliyopita ambapo taarifa zilisema kuwa walikutana
kimyakimya na kuandaa mapokezi ya Madam.
Mishale ya saa 7:00 mchana ndipo Team
Wema na mashabiki wake wengine walianza kumiminika maeneo ya
Kimara-Baruti jijini Dar wakiwa na mabasi ya kukodisha, pikipiki na
magari binafsi ambapo shamrashamra za kila aina zilifanyika.
KIBAO-KATA
Pia kulikuwa na ngoma ya Kibao-Kata, michezo ya pikipiki huku nyimbo za kumsifu Wema zikiimbwa.
Kama hiyo haitoshi, amshaamsha hiyo
ilikuwa ikifanywa kila sehemu ambapo mastaa walikuwa wakitokea maeneo
hayo kwa ajili ya kumsapoti Wema.
SHANGWE
Umati uliojitokeza walianza kulipuka kwa
shangwe baada ya kumuona Meneja wa Wema, Martin Kadinda aliyeingia
katika eneo hilo akifuatiwa na Petit Man ambaye alifuatana na wasanii wa
Bongo Fleva, Mirror na Suma Mnazareti.
MJAMZITO
Mashabiki hao wa kila kada huku watoto
wakifurika kumuona Wema walionekana kuwa na mapenzi ya hali ya juu huku
mama mmoja mwenye ujauzito mkubwa akionekana akijichanganya kila kona
bila kujali hali yake.
WEMA ENEO LA TUKIO
Wema aliingia katika maeneo hayo
(Kimara-Baruti) akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Land Cruiser ambapo
alishuka na kuingia ndani ya BMW lililoletwa kumpokea ambapo alitokea
kwenye paa na kuanza kusalimia mashabiki wake waliolipuka kwa furaha na
wengine wakiangua kilio cha furaha.
MABUSU
Kuna wengine walishindwa kujizuia wakajikuta wakimfuata Wema wakimbusu na kumshika nywele zake kama vile siyo binadamu.
CHENI NA PETE
Wema alilazimika kugawa cheni na pete
zake za dhahabu kwa mashabiki wake ili kuwatuliza huku akiwashukuru kwa
kumpokea na kuwaaga kuwa anakwenda nyumbani kwake Kijitonyama ambapo
msafara wake ulisababisha foleni ya zaidi ya robo saa njia nzima ambapo
alikuwa akisindikizwa na pikipiki.
“Yaani Madam amepokelewa na watu kama
rais vile, duh! Sijawahi kuona, amekosa ubunge lakini shamrashamra yake
kama vile ameshinda!” Alisema mmoja wa mashabiki wa Wema aliyevalia
fulana zenye nembo iliyoandikwa ‘Wema’.
KINACHOONEKANA
Habari zilieleza kwamba, kinachoonekana
Wema anajipanga upya ili kujiimarisha kisiasa kwa ajili ya baadaye hivyo
atajitahidi kuwa mbali na skendo hasa za wanaume.
TUJIKUMBUSHE
Huko nyuma Wema aliwahi kuripotiwa
kubadili wanaume mbalimbali wakiwemo; Jumbe Yusuf Jumbe, Nasibu Abdul
‘Diamond’, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ na CK.
0 Comments