humph the GREAT
Msafara
huo wa polisi ulikuwa ukitoa ulinzi kwa msafara wa mabasi ya uchukuzi
wa umma, desturi iliyoanzishwa baada ya wapiganaji hao kuteka basi moja
na kuua abiria 28 wakristu.
MAOFISA
watano wa Jeshi la Polisi nchini Kenya wameuawa leo mjini Mandera
katika shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa Kundi la Wanamgambo
la Al Shabab kutoka Somalia.
Kamishna wa jimbo hilo la kaskazini
Mashariki mwa Kenya, Bw. Job Borongo ameithibitishia kuwa wapiganaji hao
walifanya shambulizi la kuvizia dhidi ya msafara wa magari ya polisi
uliokuwa ukienda El Wak wakitumia guruneti. Maafisa hao tano waliangamia
papo hapo huku gari walimokuwa wakisafiria likiharibiwa kabisa. Maafisa
wengine wanne wamejeruhiwa vibaya.
Gavana wa Mandera, Bw. Ali Roba
aliwalaumu maofisa wa polisi katika eneo hilo kwa kupuuza tahadhari
iliyotolewa na wenyeji kuhusiana na mashambulio ya kigaidi. Roba anasema
walipuuza vyanzo vya kiintelijensia vilivyotolewa kuhusiana na
kuonekana kwa wapiganaji hao waliojihami.
Hii si mara ya kwanza Mandera kushuhudia
mashambulizi ya Al Shabaab. Shambulizi hilo la Novemba, 2014 liliwaacha
wasafiri wengi wasiokuwa waislamu na hofu ya kusafiri na hivyo
kuilazimu serikali kutoa usalama kwa mabasi ya uchukuzi wa umma. Mwezi
mmoja baadaye wapiganaji hao waliwaua wachimba migodi 36 katika eneo
hilo la Mandera.
Kundi hilo la wapiganaji wa kiislamu
limekuwa likitekeleza mashambulizi katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya
likitaka kuishinikiza taifa hilo jirani kuondoa majeshi yake nchini
Somalia. Kenya ilipeleka vikosi vyake vya jeshi nchini Somalia mwaka wa
2011 ikitaka kuzima mashambulizi ya mara kwa mara.
Hata hivyo kundi hilo limeongeza
mashambulizi nchini kenya ikiwemo mauaji ya watu 67 katika maduka ya
Westgate mjini Nairobi mwaka 2013. Mwaka uliopita Al Shabab ilitekeleza
mashambulizi katika chuo kikuu cha Garissa na kusababisha vifo vya
wanafunzi 148
Tags
HABARI