humph the GREAT

WAKALA wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (Tanzania Minerals Audity
Agency-TMAA) imejisifia namna ilivyofanikiwa kudhibiti shughuli za
uchimbaji na biashara ya madini nchini kwa kujipatia mapato stahiki
kupitia usimamizi mzuri na ukaguzi makini hasa kwa kuzingatia uhifadhi
na utunzaji thabiti wa mazingira katika maeneo ya migodi.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Gilay Shamika, alisema mbali na kujipatia mapato stahiki kutoka kwenye uzalishaji pia wakala umeweka wakaguzi maalum katika mgodi ya Williamson Diamond uliopo Mwadui, Shinyanga, unaozalisha madini ya almasi na TanzaniteOne uliopo Mererani, Manyara, unaozalisha madini ya Tanzanite.
Alifafanua kuwa katika kipindi cha Julai 2015 hadi Machi 2016, kiasi cha karati 119, 218 za almasi zenye thamani ya Dola za Marekani 56,709,683.28 ziliuzwa na kulipiwa mrabaha wa dola za Marekani 2,774,085.78.
Aliongeza kwamba mbali ya kudhibiti eneo la uzalishaji, wakala pia kwa kushirikiana na jeshi la polisi, TRA, TAA, Idara ya Madini na Usalama wa Taifa umeweka wakaguzi katika viwanja vya ndege na mipaka ili kudhibiti biashara haramu na utoroshaji wa madini nchini.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Ukaguzi wa Madini, Gilay Shamika (kulia) akisoma taarifa kwa
wanahabari. Pembeni mwake ni baadhi ya viongozi wenzake wa Wakala wa
Ukaguzi wa Madini.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Gilay Shamika, alisema mbali na kujipatia mapato stahiki kutoka kwenye uzalishaji pia wakala umeweka wakaguzi maalum katika mgodi ya Williamson Diamond uliopo Mwadui, Shinyanga, unaozalisha madini ya almasi na TanzaniteOne uliopo Mererani, Manyara, unaozalisha madini ya Tanzanite.
Alifafanua kuwa katika kipindi cha Julai 2015 hadi Machi 2016, kiasi cha karati 119, 218 za almasi zenye thamani ya Dola za Marekani 56,709,683.28 ziliuzwa na kulipiwa mrabaha wa dola za Marekani 2,774,085.78.
Aliongeza kwamba mbali ya kudhibiti eneo la uzalishaji, wakala pia kwa kushirikiana na jeshi la polisi, TRA, TAA, Idara ya Madini na Usalama wa Taifa umeweka wakaguzi katika viwanja vya ndege na mipaka ili kudhibiti biashara haramu na utoroshaji wa madini nchini.
Alifafanua pia kwamba ukaguzi uliofanywa na
TMAA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania uliwezesha baadhi
ya kampuni za uchimbaji kuanza kulipa kodi ya mapato na kipindi cha
mwaka 2009 hadi Machi 2016, kampuni mbalimbali zililipa jumla ya
Shilingi bilioni 732.6 kama kodi ya mapato.
Tags
HABARI