humph the GREAT
Rihanna akibubujikwa na machozi jukwaani.
NYOTA
wa muziki kutoka marekani Rihanna alibubujikwa na machozi wakati wa tamasha mjni Dublin
usiku wa kuamkia jana baada ya kuwasili akiwa amechelewa kwa dakika 30
katika ukumbi huo.
Mwanamuziki huyo alijawa na
hisia wakati alipoanza kuimba wimbo wa ‘Love The Way You Lie’ aliyoimba
kwa ushirikiano na mwanamuziki Eminem.
Mashabiki waliweka picha na video za
mwanbamuziki huuo katika mitandao ya kijamii wakionyesha wasiwasi wao
kuhusu kile kilichotokea.
Rihanna
hakuelezea ni nini kilichotokea mbali na kuandika ujumbe kwatika
mtandao wake wa Instagram akiusifu usiku huo,ilikuwa tamasha iliojaa
hisia kwambgu,aliandika.
”Nina bahati kuwa na kikosi kama vile #Navy man,nimebarikiwa.Ninashukuru sana kwa kuwa nanyi nyote”.#DUBLIN#ANTIWORLDTOUR”
Rihanna atakuwa nchini Uingereza katika
uwanja wa Webly siku ya Ijumaa.Wakati alipozindua albamu hiyo
,alionekana akiangalia kando na kamera na kuinua mikono kama ishara ya
kutaka kujizatiti.
Lakini mashabiki wake waliokuwa
wamefurika katika tamasha hilo waliendelea kumuimbia hadi akafuta
machozi yake na kuendelea na dakika 80 za kuwatumbuiza.
”Sijawahi kusikia watu wakipiga kelele kwa sauti ya pamoja na hilo limetokea Ireland mjini Dublin”,aliuambia umati.
Tags
Michezo na burudani