humph the GREAT
khadija nito
DAR ES SALAAM: Msanii wa kike wa
Bongo Fleva ambaye kwa sasa anasumbua na wimbo wake wa One More Night,
Hadija Maige ‘Kadja Nito’ anadaiwa kupigwa ndoa ya fasta siku chache
baada ya Mfungo wa Ramadhani kuanza.
Chanzo ambacho ni rafiki wa msanii huyo
kilitung’ata sikio kuwa, Kadja ambaye ni mama wa mtoto mmoja alikuwa na
jamaa yake ambaye alimuomba amuoe kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani ili akampikie futari, mambo yakaenda sawa na ndoa ikafungwa
kimyakimya.
Baada ya kunasa ubuyu huo, paparazi wetu
alimvutia waya Kadja na kumuuliza kuhusu jambo hilo la heri ambapo
alifunguka: “Mmh! Yaani ninyi bwana, mimi siyo wa kuolewa ndoa ya
futari, halafu nachukia sana kufuatiliwa mambo yangu binafsi.
“Mambo ya ndoa sasa hivi yanakujaje, wewe niulize nina wimbo gani mpya, naendeleaje na swaumu, hapo sawa.”
Tags
wasanii