Watoto wa mitaani Arusha kujengewa hostel

humphrey the GREAT

Baadhi ya Watoto wa mitaani waishio jijini Arusha waliokusanywa na taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto wa mitaani kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao
Watoto wa mitaani wanaoishi jijini Arusha katika mazingira hatarishi wanatarajiwa kujengewa Hostel zitakazowasaidia kuondokana na adha ya kupata sehemu za malazi hivyo kulazimika kulala maeneo ya stendi za mabasi na masoko.
Mkurugenzi wa shirika la Gola linalojihusisha na masuala ya watoto wa mitaani jijini Arusha,Sawale Maghema  amesema kuwa mpango huo utasaidia watoto wa mitaani kuondokana na mazingira magumu yanayowapelekea kujiingiza katika vitendo vya uhalifu na matumizi ya madawa ya kulevya.
Sawale alisema kuwa iwapo watoto wa mitaani watatelekezwa na jamii bila kusaidiwa wanaweza kugeuka na kuwa mwiba kwa jamii ya Watanzania hivyo amewataka Watanzania kujitokeza kuwasaidia watoto hao .
“Watoto wa mitaani tuna mpango maalumu wa kuwakusanya na kuwakutanisha pamoja kujua mahitaji yao ,malengo na matarajio waliyonayo ili kuwasaidia kwa kushirikiana na jamii hata kwa hili la ujenzi wa Hostel litasaidia kuwaweka pamoja tukiwaacha waendelee kukaa mitaani hawatabadilika wataendelea kuwa na maisha mabaya” Alisema Sawale.
Mdau wa Masuala ya utalii Mustafa Panju  alijitolea kuwasaidia watoto wa mitaani kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 20 kwa watoto hao ili waweze kupata mahitaji muhimu
Ameeleza kuwa jamii inapaswa kuamka na kuwasaidia watoto hao badala ya kuwaacha waendelee kukaa kwenye mazingira hatarishi.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Arusha , Hassan Omari akizungumza kwa niaba ya watoto wa mitaani anaeleza kuwa watoto wa mitaani wana ndoto nyingi,vipaji na uwezo wa hali ya juu hivyo wakisaidia wanaweza kufika mbali na kulisaidia taifa.
Chanzo: Libeneke la Kaskazini



Tan

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post