humph the GREAT
\
\
STAA wa Bongo Fleva ambaye ni
zao kutoka jumba la kuibua vipaji (THT), Khadija Said ‘Kadjanito’
ameamua kujiingiza rasmi kwenye filamu.
Akizungumza na mtandao wa Global Publishers, Kadjanito
anaye-tamba na Ngoma ya One More Night alisema kuwa kuigiza ni kipaji
alichokuwa nacho tangu zamani na kwamba ndoto yake ilikuwa kwanza
kuanzia kwenye muziki.
“Napenda sana kuigiza haimaanishi kwamba
muziki nimeacha, noo! Siwezi, kwa sasa nimeona tu napo kwenye filamu
nina uwezo. Ndiyo kwanza nimetoka kambini kushuti filamu mpya inakuja
(jina limehifadhiwa) na mashabiki wakae mkao wa kuniona kwenye filamu
nyingi za Kibongo (Bongo Muvi),” alisema Kadjanito.
Tags
Burudani