humph the GREAT
Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20 Percent akishuhudiwa na Wakili msomi, Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na Meneja Uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye Studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za 20 Percent.
20
Percent akipongezana na producer Mann Water baada ya kuwekeana saini
mkataba wa kufanya kazi pamoja chini ya lebo ya KOMBINENGA kwenye studio
za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam. (Picha na
Sultani Kipingo)
Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20 Percent akishuhudiwa na Wakili msomi, Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na Meneja Uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye Studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es Salaam.
Na Humphrey eno, blogger
Mfalme wa Afro Pop nchini Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20 Percent
amevunja ukimya na kurejea kwa kishindo kwenye anga ya muziki, huku
akiwa msanii wa kwanza kusaini mkataba na lebo mpya ya KOMBINENGA
inayoendeshwa na producer nguli John Shariza a.k.a Mann Water.
20 Percent, ambaye
mwaka 2011 alitwaa tuzo saba za Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kwa
mpigo, huku Mann Water akisomba tuzo mara mbili mfululizo za producer
bora (mwaka 2013 na 2014), tayari amesharekodi vibao vitano na
anatarajia kuachia ngoma moja mpya ya kwanza Julai 18, 2016, katika
kuandaa albamu yake ya SAUTI YA GHARAMA.
“Nimerudi kuwachinja tena” anasema 20 Percent,
akiwa anakamilisha kurekodi katika studio za Combination Sounds iliyoko
Kinondoni Sounds jijini Dar. “Nimerudi kurudisha sauti ya gharama kwa
jamii. Sauti inayofundisha. Sauti inayoonya. Sauti inayoburudisha. Sauti
inayozengua kila mtu, ” anaogeza.
Tayari 20 Percent
ameshasaini mkataba wa miaka mitano na lebo ya KOMBINENGA, katika hafla
fupi iliyofanyika Jumapili katika ofisi za Combination Sounds. Kuanzia
sasa shughuli zote za msanii huyu zitasimamiwa na lebo hiyo chini ya
Producer Mann Water.
Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha
Attorneys ndiye aliyefanikisha zoezi hilo la kutiliana saini mkataba
lililoshuhudiwa pia na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel
Moses.
“Namkubali sana 20 Percent
ni msanii aliyetimia na hutumii shuruba wakati wa kurekodi maana ana
kipaji cha ajabu cha kutunga akiwa wima na kukariri hapohapo”, anasema
Mann Water, ambaye ameshafanya kazi na wasanii nyota kibao wakiwemo
Lady Jay Dee, Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Christian Bella, MB Dogg, Juma
Nature, Mr Blue na wengine wengi.
20 Percent alitamba
sana tokea mwaka 2006 kwa wimbo wake wa “Manemane” uliomfanya ashinde
tuzo ya KTM, kabla ya kuweka historia ya kusomba tuzo saba kwa mpigo
mwaka 2011. wakati huo nyimbo zilizompandisha chati zilikuwa ni “Tamaa
Mbaya” na “Ya nini Malumbano” na “Maisha ya Bongo”
Mbali na Muziki 20 Percent pia alitamba sana kwenye tasnia ya filamu ambapo alicheza kwenye mchezo uliofahamika kwa jina lake la 20 Percent.
Baada ya hapo akaamua kupumzika kwa muda na kujishugulisha na shughuli
za kilimo. “Kilimo kinaendelea vyema na sasa nimeamua kurudi kwenye gemu
ili kuwachinja tena” alimalizia, akiinuka kuelekea kwake Kimzichana,
Mkuranga, Mkoa wa Pwani, anakoishi.
Tags
Burudani