humph the GREAT
Huu hapa ni kusanyiko wa picha za mitindo na tamaduni zilizovutia watu sana katika mitandao ya kijamii wakati wa sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Rio, 2016.
- Mavazi ya kitamaduni … na viatu kutoka Burundi
- Shelly-Ann Fraser-Pryce kutoka Jamaica aling'aa kwa mtindo wake wa nywele
- Wanamichezo kutoka India nao walivutia kwa koti zao na sari
- Ureno mtindo wao ulikuwa wa jeans
- Indonesia waliamua kuvalia kifalme
- Bermunda nao wakavumisha kaptula za Kibermunda
- Mbeba bendera huyu wa Tonga alisisimua wengi kwa kifua chake wazi kilichong'aa kutokana na mafuta
- Norway walitikisa ukumbi kwa vazi hili
- Kwa Msumbiji, mashati yenye michoro ya vijisanduku ndiyo yalikuwa mavazi ya sherehe
Tags
Burudani