humph the GREAT
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesitisha malipo ya posho za kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini ambao wanaofanya mafunzo kwa vitendo (practical training) ‘field’ baada ya kubaini kuwepo na wanafunzi hewa zaidi ya 1000 vyuoni.

Prof. Ndalichako amesema wizara yake
imezuia posho hizo kwa muda wa wiki mbili wakati wizara hiyo ikiwa
inafanya uhakiki ili kuwabaini wanafunzi hewa zaidi pamoja na wahusika
kuwachukulia hatua za kisheria.
Aidha Prof. Ndalichako amewaagiza wakuu
wote wa vyuo kuwasilisha taarifa za wanafunzi wao wizarani ili zoezi la
kukagua na kubaini uahalali wa wanafunzi hao kuwepo vyuoni na wale
watakaoonekana kuwa wana sifa watapatiwa posho zao za kujikimu mapema na
kuendelea na masomo.
Tags
HABARI