humph the GREAT
TIMU ya soka ya Simba jana ililazimishwa sare ya bao 1-1 na URA ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
TIMU ya soka ya Simba jana ililazimishwa sare ya bao 1-1 na URA ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Simba imepata matokeo hayo, ikiwa ni wiki moja baada ya kuifunga AFC Leopards ya Kenya mabao 4-0 katika mechi ya kuadhimisha tamasha la Simba Day Agosti 8 mwaka huu.
Wageni walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza katika dakika ya 19 baada ya Nkugwa Elkanah kuunganisha krosi ya Kagimu Shafiq na kuujaza wavuni mpira.
Kuingia kwa bao hilo kulizidisha makali kwa wachezaji wa timu zote na katika dakika ya 30 nusura Shiza Kichuya aisawazishia Simba bao hilo lakini shuti lake lilipanguliwa na kipa wa URA, Muwanga Mathius.
Dakika mbili baadaye nahodha wa Simba, Jonas Mkude aliisawazishia timu yake bao hilo baada ya kuunganisha pasi ya Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ aliyepiga mpira wa adhabu nje ya 18 na kumkuta mfungaji aliyeuunganisha nyavuni.
Kwa ujumla katika mechi hiyo, timu hizo zilishambuliana kwa zamu na kujikuta zikimaliza dakika 90 na matokeo hayo ya sare ya bao 1-1. Aidha mechi hiyo pia ilitumika kumuaga mshambuliaji wa siku nyingi wa Simba, Mussa Hassan Mgosi ambaye sasa amekuwa meneja wa timu hiyo.
Mgosi aliingia uwanjani na wachezaji wa timu hiyo akiwa amevaa jezi kama kawaida ambapo alicheza kwa dakika tano kabla ya kutolewa na kukabidhi kitambaa cha unahodha kwa Jonas Mkude aliyebeba mikoba hiyo.
Baada ya hapo, Mgosi ambaye wakati akikabidhi kitambaa cha unahodha alishuhudiwa pia na familia yake (mke na watoto watatu) kisha Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alimtambulisha rasmi kuwa anastaafu na atakuwa meneja wa timu, kisha akaingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kutoka akiwa amebadili na kuvaa mavazi ya kawaida.
Mbali na kuchezea Simba kwa mafanikio kwa nyakati tofauti, Mgosi pia amewahi kuzichezea JKT Ruvu, Mtibwa Sugar na Motema Pembe ya Congo DR.
Tags
Michezo na burudani