humph the GREAT
Kufuatia kuandikwa rasmi kwa Sera ya Taifa ya Utamaduni na iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni chini ya Waziri Profesa Juma Kapuya mwaka 1997, kumekuwa na ongezeko kubwa la wadau wa sanaa na burudani wakitaka kujihusisha na matukio au shughuli mbalimbali katika sekta hii.
Ongezeko hili kwa kiasi kikubwa limetokana na kufunguliwa milango kwa wafanyabiashara na wadau binafsi wenye maslahi mbalimbali kuingia katika sekta ya sanaa.
Kimsingi huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuzaliwa kwa matukio mbalimbali ya sanaa na burudani ambayo mengine bado tunaendelea kuyashuhudia hadi leo, lakini mengine yakiwa yanasuasua na baadhi kujifia.
Kwa upande mwingine, sera hiyo ya utamaduni sanjari na kufungua milango kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali kujihusisha na shughuli za sanaa na burudani ililiacha Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na mamlaka ya kusimamia na kuiratibu sekta ya sanaa.
Lengo likiwa ni kuhakikisha kila kitu kinakwenda kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi, lakini pia zile zilizoandaliwa na kuridhiwa na wadau katika mchakato wa tukio au shughuli husika.
Msingi wa hoja hapa ni kwamba, kuwepo kwa wadau wa sanaa hususan wafanyabiashara wanaojihusisha na sekta hiyo lazima kuende sambamba na uwepo wa uratibu makini wa sekta hii muhimu kwa uhai wa taifa lolote.
Lengo ni kuhakikisha kwamba kunakuwa na mazingira rafiki kwa wadau wote, lakini pia kuweka taratibu na kanuni ambazo siyo tu zitaleta tija, katika sekta lakini pia kujenga dhana ya uwazi na uwajibikaji unaojali haki, usawa, weledi na maadili.
Moja kati ya maeneo ambayo Basata imeyatilia mkazo ukiacha ile ya kubadili na kuhuisha muundo wake wa utawala na menejimenti, ni kujenga misingi makini ya utawala wa sekta ya sanaa, lakini pia kujenga nyenzo za kuwasimamia na kuwaratibu kwa ukaribu wadau wote wanaojihusisha na sekta ya Sanaa.
Misingi iliyojengwa na Serikali kupitia sera hii ya Utamaduni ndiyo leo hii imeamsha ari ya vijana wengi kujikita kwenye sekta ya sanaa na burudani, lakini kuibuka kwa wafanyabiashara na kampuni zinazoona fursa katika sekta hii.
Kazi kubwa ya Basata ni kujenga mazingira rafiki kwa wadau wote wa sanaa wakiwamo wasanii na wakuzaji sanaa (mapromota), kufanya kazi zao kwa kuzingatia haki na maslahi bora lakini pia kutanguliza sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za uendeshaji na uratibu.
Ieleweke kwamba, msanii kama mdau mkuu kwenye sekta ya sanaa hawezi kusimama peke yake katika kusukuma sekta.
Yeye atabaki na kipaji au weledi utakaomwongoza katika kubuni kazi za sanaa na atawahitaji wakuzaji sanaa (mapromota) katika kupata fursa za matamasha, mashindano, tuzo mbalimbali baada ya kufanya makubaliano maalumu ya mkataba.
Kwa mujibu wa sera iliyopo ya utamaduni ya mwaka 1997 na mabadiliko ya mifumo ya kiuchumi na uzalishaji yaliyolikumba taifa na dunia kwa ujumla, dola lililazimika kufungua milango kwa sekta binafsi na lenyewe kubaki na usimamizi, utunzi wa sera, sheria na taratibu za usimamizi wa sekta mbalimbali.
Tasnia ya sanaa nayo haikubaki salama. Iliathirika na mabadiliko hayo ya kisera katika uchumi na uzalishaji kwa ujumla.
Kwa hiyo, Basata kwa mamlaka iliyopewa kisheria ya kuisimamia sekta ya sanaa nchini, imekuwa wakati wote likisimamia utekelezaji wa sera ya utamaduni na kuhakikisha wadau wote wanajielekeza katika jukumu hili kupitia uzingatiaji wa sera yenyewe lakini pia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali.
Ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa Basata limekuwa likitoa fursa sawa kwa wadau wote wa wenye nia na dhumuni la kuwekeza kwenye sekta hii.