Q Chief aeleza vitu ambavyo havifurahii ndani ya ‘label’ ya QS Mhonda

humph the GREAT
 Q Chief  
Msanii wa muziki Q Chief amesema ingawa anafanya kazi na label ya ‘QS Mhonda Entertainment’ lakini kuna vitu ambavyo havimfurahishi ndani ya ‘label’ hiyo.

Muimbaji huyo ambaye aliachia wimbo ‘Mkungu wa Ndizi’ akiwa amemshirikisha TID, ameiambia Bongo5 kuwa bosi wake amekuwa mzito katika maamuzi mbalimbali ya kazi.

“Najua nimeahidi video, kampuni iliniahidi kunipeleka Afrika Kusini lakini mpaka leo ninavyozungumza bado kuna mvutano. 
Kwa sababu mkurugenzi ana watu wengi ambao wanampa maoni”, alisema Q Chief
Aliongeza,”Kwa hiyo pengine kuchelewa ni vizuri kwa sababu na mimi naona kazi za watu wengine na najua nibadilike vipi, lakini unavyoachia hit na video inatakiwa kutoka. Ninapotoa ahadi kwamba video inakuja alafu haipo tatizo linakuwa kwangu, naonekana siko organized”

https://youtu.be/U0DBlnLOOac 

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post