humph the GREAT
MZAZI mwenzake na staa wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa
Mitego’, Siwema ameibuka na kutoa simulizi yake ya nyuma na kusema kamwe
hatasahau mzazi mwenzake huyo alivyomuongopea na kumpiga shilingi
milioni 7 taslimu.
Siwema aliivujisha ishu hiyo hivi karibuni wakati mwanahabari wetu
alipomtaka aseme kitu gani ambacho hatakisahau kutoka kwa mpenzi wake
huyo wa zamani ndipo mrembo huyo alipofunguka hayo lakini akasema hata
hivyo, alishasamehe kwa sababu yalitokea kwenye kipindi ambacho penzi
lilikuwa motomoto.
“Si unajua tena mtu ukikolea, kuna kipindi aliniambia ametaitiwa polisi,
zinahitajika hela, nilipata mshtuko kweli, ikabidi niende benki haraka,
nikamtumia. Nilishasamehe maana tuliyazungumza na tukiwa kama wapenzi
yaliisha, ila sitasahau aisee,” alisema Siwema.
Alipotafutwa Nay ili kumsikia kama ana lolote kuhusu ishu hiyo, simu
yake iliita kwa nyakati tofauti bila kupokelewa kwa takriban wiki tatu
mfululizo.
Tags
Udaku