humph the GREAT
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kuwa msimamo wake wa
kupinga kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Magufuli cha kuzuia mchanga wa dhahabu kusafirishwa nje uko pale pale.
Ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma, ambapo amesema kuwa kuzuia mchanga
huo wa dhahabu kusafirishwa kwenda nchi za nje kutaathiri uchumi kwani
atakuwa ameenda kinyume na mikataba ya kimataifa.
“Rais Dkt. Magufuli amefanya kitendo ambacho ni kinyume na mikataba ya
kimataifa, kwa hiyo hapa tutegemee hasara kubwa na kutengwa na jumuiya
ya kimataifa,”amesema Lissu
Tags
HABARI