humph the GREAT
BABA wa watoto wawili amefichua kwamba hunywa glasi ya mkojo wake
mwenyewe kila siku na anausifu kwa kumwezesha kupunguza uzito kwa kilo
50.
Kwa kipindi cha miaka sita iliyopita, Dave Murphy (54) mkazi wa
Basildon, Essex nchini Uingereza amekuwa akinywa mkojo wake, anaosema
kuwa unahusika si tu kupungua kwa unene wake bali pia kumletea mwonekano
wa ujana na siha njema.
Dave, ambaye aliweza kupunguza uzito kutoka kilo 127 hadi kilo 76 kwa
tiba hiyo, pia anaamini mkojo unaweza kuwa suluhu ya uhaba wa chakula
duniani na kuweza kubana matumizi kwa wanaofuja fedha baa.
Sehemu kubwa ya siku, Dave hutumia pesa kidogo kwa mlo, ambao pia unahusisha chungwa moja na glasi mbili za mkojo wake mwenyewe.
Kile anachopenda zaidi ni sehemu ndogo ya chips kutoka duka lililo jirani, ambazo huagiza mara tatu kwa wiki.
Wakati fulani mwaka 2012 kwa kipindi cha siku 30, Dave hakula kitu kingine chochote zaidi ya mkojo wake.
Dave pia hutumia mkojo wake kunawa uso na kuogea na anasisitiza kuwa mkojo ni bidhaa muhimu ya kuzuia hali ya kuzeeka.
Dave anaeleza: “Baada ya kunywa mkojo wangu, nilijihisi kuwa na afya na
mkakamavu kuliko nilivyokuwa kabla na nilipunguza uzito wa kilo 50.
“Zaidi ya hayo, sihitaji fedha zaidi ili kuishi kwa sababu ninachotumia
ni mkojo niunywao, ambao unanifanya nisiwe na haja ya kula chakula
kingi.
“Kama wanadamu, hatupaswi kutumia kiasi kikubwa kama hicho cha chakula.
Mkojo unaweza kutusaidia kupunguza kile tunachohitaji kuingiza tumboni –
maana ndani yake kuna kila kitu binadamu anachohitaji.
“Watu wengi wanadhani mkojo wakiunywa ni uchafu lakini si hivyo. Kiuhalisia ni msafi kuliko maji.
“Mkojo ni taswira ya kile ambacho mwili wako unahitaji lakini umezidi zaidi kimanufaa.
“Kwa mfano, iwapo una maambukizo kisha mkojo wako utakuwa na silaha za
kupambana nazo. Huboresha mfumo wa kinga na hata kuponya pumu
iliyonisumbua kwa muda mrefu wa maisha yangu.
“Tiba ya mkojo si kuhusu kuunywa tu, unaweza kuogea na kujipaka. Ni
bidhaa inayozuia ngozi kuzeeka – mikunjo na makunyazi yaliyokuwamo
ngozini mwangu usoni na kwingineko mwilini imetoweka tangu nilipoanza
kutumia mkojo wangu kuogea na kunawia.
“Unawea kuutumia hata kuondoa maumivu au muwasho na kama vile ya macho.
“Mkojo ni tiba kwa kila kitu. Iwapo watu watabadili mtazamo wao kuhusu
tiba hii, hakika kisha kila mtu atashuhudia maajabu na manufaa makubwa
ya maji haya kutoka mwilini mwetu.”
Dave alianza matumizi ya mkojo Mei 2011 baada ya awali kusita sita kabla ya kuhudhuria mkutano kuhusu tiba ya mkojo.
Je, kweli mkojo hufanya kazi?
Tiba ya mkojo inaelezwa kurudi nyuma nyakati za Biblia na nyaraka za
kihistoria zinaeleza namna ulivyokuwa ukiponya majeraha yaliyoambukizwa
na manufaa yake pia yameandikwa katika riwaya za Kihindi na Kichina.
Mkojo kwa kiasi kikubwa ni msafi, ukiwa na asilimia 95 ya maji na
asilimia tano ya virutubisho kama vile protein, vitamini na madini.
Madini hayo ni pamoja na urea, chloride, sodiamu, potassiamu na chuma.
Baada ya kula na mmeng’enyo wa chakula kufanyika, maji pamoja na mabaki yaliyomeng’enywa husafirishwa katika kibofu cha mkojo.
Maji hayo ndiyo husaidia kufanya usafirishaji wa mabaki hayo hadi katika kibofu cha mkojo.
Aidha, wakati wa mchakato wa usagishaji, maini hushughulika na sumu na kuziondoa.
Kisha damu inaenda katika figo, ambako huchujwa tena na vitu
visivyohitajika mwilini hukusanywa katika mchanganyiko wa maji ambao
hutoka kama mkojo.
Lakini Dk. Rob Hicks alisema: “kwa miaka mingi watu wengi walidai uwapo
wa faida za kiafya kwa kunywa mkojo wao, lakini kwa kadiri nijuavyo
hakuna ushahidi wa kisayansi kuunga mkono madai hayo.
“Figo ni mfumo fanisi wa uchujaji wa kuondoa taka mwilini na hiyo ni
kazi yake ya asili. Binafsi naamini kuna njia nzuri zaidi na isiyoleta
kinyaa za kuufanya mwili kuwa na afya ikiwamo kutovuta sigara, kula mlo
bora na kutoruhusu msongo wa mawazo.”
Lakini Dave anakumbushia jinsi alivyokuwa na uzito mkubwa huku akiwa na
afya mbovu ikiwamo kusumbuliwa na pumu tangu utotoni, kitu ambacho tangu
atumie mkojo kimetoweka.
Anaeleza: “Miaka sita iliyopita nilikuwa na uzito mkubwa na mgonjwa sana, nilitumia steroids kuikabili pumu.
Nikiwa nafanya kazi kama mtaalamu wa program za kompyuta katika Jiji la
New York, mlo wangu ulitisha. Ungeniona nikila chocolate siku nzima
achilia mbali chakula cha mchana na usiku.
“Wakati nilipotania kwa kuzungumzia tiba ya mkojo na wafanyakazi
wenzangu wakati wa tamasha moja, kiukweli sikuwa na lengo hilo. Lakini
mwishowe tukaamua tujaribu!”
Tangu hao nikaanza kunywa glasi ya mkojo mara mbili kwa siku. Pamoja na
kuwa muwazi kuhusu hilo, anakiri awali alisita na kuona kinyaa kunywa
mkojo wake mwenyewe kabla ya kuzoea.
Dave anasema tangu hapo akazoea na kuona ni jambo zuri na matokeo ya
unywaji mkojo wake ni kupungua uzito, kuwa na siha ya ujana pamoja na
maradhi ya pumu kumtoka.
Ukiachana na hilo mkojo mbali ya kuelezwa kuwa na manufaa kiafya,
wanayansi na watafiti Uingereza wameshavumbua nguvu za mkojo katika
kuzalisha nishati ambayo inaweza kuchaji simu kwa muda wa dakika 25 na
pia kumwezesha mteja kutuma ujumbe na kuperuzi intaneti.
Mbali ya hilo hivi karibuni watafiti nchini Ujerumani wamedai kutengeneza pombe kutokana na mkojo.
Download Udaku Special App K
Tags
HABARI