humph the GREAT
Baada ya Young Killer kutoa 'dis track' aliyoipa jina 'True Boya' kumhusu Nay wa Mitego ambaye alimchana kupitia ngoma yake mpya 'Moto' Nay ameijibu kwa kukazia alichokiimba kwenye ngoma yake ni ukweli uliopo mtaani kwa mashabiki na wadau wa muziki.
Baada ya Young Killer kutoa 'dis track' aliyoipa jina 'True Boya' kumhusu Nay wa Mitego ambaye alimchana kupitia ngoma yake mpya 'Moto' Nay ameijibu kwa kukazia alichokiimba kwenye ngoma yake ni ukweli uliopo mtaani kwa mashabiki na wadau wa muziki.
Nay
amefunguka na kusema kwamba hata diss track aliyoitoa Young Killer ni
jingle kwani wimbo haujakamilika ingawa kwa upande wake alikuwa serious
wakati anamchana kwa kuwa ni kweli hana makali kama aliyokuwa nayo awali
wakati anatoka.
"Wimbo alioutoa Young Killer
nimeusikia vizuri lakini kwangu ni jingle kwa sababu haujakamilika.
Mimi nipo Serious na nilichokiongea kwa sababu watu wanaongea kwamba
ana'drop'. Sasa kama kuongea ukweli ni kuchamba basi tutakuwa wengi sipo
mwenyewe. Ni kweli kuandika anaandika vizuri lakini ni kama karudi
hatua nyingi nyuma. Ninachozungumza mimi hata yeye anakijua na hata
wadau wa muziki wanaelewa" Nay alifunguka.
Aidha Nay ameongeza kwamba
"Wasanii kama Baraka na Young Killer warudi nyuma wajue ni wapi
walikosea na waombe radhi kwa watu waliowatambulisha kwenye game kama
hawapo nao sawa. Kama mtu alitoa muda wake hata kwa dakika kwa ajili ya
kufanya jambo kwa ajili yako alafu baadae ukawa hauko nae sawa unatakiwa
urudi nyuma na kujua wapi umekosea kwani hujui mtu alipoteza muda kiasi
gani. Siku zote Discipline ndio kila kitu hivyo wajifunze" aliongeza Nay.
Pamoja na hayo Nay ameongeza kwamba
upepo wa ngoma ya 'Muziki' aliyoifanya rapa Darassa haikumpatia Stress
kwa sababu hata yeye aliwahi kuwa na hit song nyingi na bado ataendelea
kuzitoa kila siku.