Ambacho mabinti kustuka, ni kwamba wengi wataolewa na bodaboda, wafanya biashara, na ukibahatika sana na mwanasiasa kwa sababu wasome wengi hivi sasa hawana ajira hivyo atakwambia ngoja kidgo nipate ajira mpenzi, utazeeka unamsubiri.
Lakini pia kumbuka binti mzuri ni kati ya miaka 22, 23, 24 na 25.
kwa mliofika chuo basi 26, 27 na 28, ukifika miaka29 huwa ni mstari mwekundu hapa unaweza angukia kwa mzee wa miaka 52.
Ni vizuri binti uzae kati ya miaka 20 hadi 35 ukomo wake kwa maana ya kufunga kizazi na kuanza kulea familia na majukumu mengine ya kumaisha pamoja na kula ulivyoviandaa.
Ukivuka miaka 35ujue umasikini hautaumaliza yaan ununue nepi una miaka 45, vilevile inategemeana na afya yako pia.
Ninyi wanaumeumemaliza degree ya kwanza una miaka 26, 27, 28 au 29 kwa sasa bado unasema unajipanga huwezi oa sasa hivi, Leo mtu anakufa kwa kuanguka tuu kama papai , huna mtoto historia ya marehemu huwa haichekeshi bali huzua walakini!!!
Kukaa unaende nje na kutongoza tongoza tuu bora uoe ndugu yangu kama maisha sote tunayatafuta tuu mbona.
Hakuna siku unayosubiri eti ujuenge nyumba, uwe na gari au ufanye kitu kiongine kikubwa, wewe oa mtafute na mkeo huenda akakupa mawazo ambayo yatakupeleka mbali zaidi ya hapo ulipo kaka yangu..
Hivyo ndugu zangu sisemi muoe au msioe la hasha, ELIMU YAKO ITATHAMINIWA SANA UKIOA AU KUOLEWA...
0 Comments