Je, wewe ni mshambuliaji wa kimo cha futi sita inchi moja? Unaweza kupata kazi Chelsea

humph the GREAT
Andy Carroll, Christian Benteke, Peter Crouch, Ashley Barnes na Edin DzekoHaki miliki ya pichaPA, GETTY
Image captionAndy Carroll,            Christian Benteke,     Peter Crouch,            Ashley Barnes            na Edin Dzeko
Mchezaji anayetafutwa ni lazima awe na urefu wa futi sita inchi moja, awe na uzoefu wa ligi ya EPL , umri na kasi yake sio muhimu lakini atahudumu kwa mkataba wa muda mfupi.
Chelsea bado hawajaweka tangazo hilo katika gazeti lolote magharibi mwa London mwezi Januari lakini kuna wakati ambapo utafutaji wa mshambuliaji ulionekana kuwa wa kukatisha tamaa
Yamkini wanawatafuta wachezaji warefu wa kimo.
Andy Caroll, Ashley Barnes, Islam Slimani na Peter Crouch ni miongoni mwa wachezaji wanaohusishwa na uhamiaji wa kuelekea kwa mabingwa hao watetezi.
Mpango wao wa kumtafuta mshambuliaji huyo mrefu kwa kimo na ambaye atakuwa kwa mkopo ama kwa mkataba wa kudumu - umesababisha hali ya eti eti katika mitandao ya kijamii huku wachezaji nyota wa zamani wa mchezo huo wakitania kwa kutangaza kwamba wamejiondoa kutoka kwenye orodha ya wanaotafuta kazi Chelsea.
Gary Lineker tweetHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionGary Lineker aliandika kwamba ni mfupi mno kiasi kwamba hawezi pewa kazi Chelsea
Adebayo Akinfenwa tweetHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionMshambuliaji wa Wycombe Adebayo Akinfenwa ni miongoni mwa waliotania hatua hiyo ya Chelsea
Mshambuliaji wa Roma na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Manchester City Edin Dzeko aliibuka kuwa mchezaji anayefaa ikilinganishwa na Lineker na Akinfenwa.
Lakini umri wake utafikia miaka 32 mwezi Machi, hawezi kushiriki katika Kombe la Klabu Bingwa Ulaya na bei yake ya £44m ikiwa katika mpango wa kubadilishana na beki wa kushoto Emerson Palmieri, ilifanya watu kuanza kuuliza lengo la uhamisho huo.
Miongoni mwa wale walioshangazwa ni wachezaji wa Chelsea wenyewe.
Eden Hazard ambaye amekuwa akicheza katika safu ya mashambulizi amesema kuwa Chelsea haihitaji mshambuliaji msimu huu, hususan 'mshambuliaji''.
Mchezaji huyo wa Ubelgiji alisema: Ni klabu gani bora msimu huu, Manchester City, washambuliaji wake sio warefu kwa kimo.
''Ni rahisi, iwapo unataka kucheza mpira wa pasi ndefu, unahitaji kulenga mtu na iwapo unataka mpira kuchezwa sakafuni, unahitaji watu wafupi.
Hivyo basi ni kwa nini mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte amejitahidi kuhakikisha kuwa anamsajili mchezaji wa ziada wa Alvaro Morata, na ni kwa nini kuna orodha kubwa ya majina?
BBC michezo inamuuliza mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Chris Sutton nani anafaa - na hatma ya klabu hiyo.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post