Baada ya kumaliza kuongea na asia kwa simu nilirudi nilipokuwa nimemuacha baba na sikumuona tena baba pale alipo kuwa amekaa ndipo nikazidi kuchanganyikwa na ghafra umeme ukazima nikaanza kusikia vicheko vya watu kutoka ndani na nje ya nyumba hapo nikaona kama giza kichwani mwangu na macho yakawa mazito nikajiona kama naelea hewani hivi huku miguu imekufa gazi, nakaona naonana na watu wa aina tofauti tofauti baadae ukimya ukatanda kila kona na nikiwa peke angu sielewe ni wai nilipo ninapoelekea wala ninapokanyaga, ghafra ukapita mwanga mkali machoni kwangu...
SONA NAYO.....
Kwa muda mfupi nilijikuta kama akili haifanyi kazi na sio akili tuu karibu viungo vyote vya mwili vilisimama na nikajikuta mapigo ya moyo yanazidi kuongeza spidi bila kuelewa nini nifanye nikajikuta kwa muda mfupi najilaumu kwanini nilikuwepo duniani mbna kama matatizo yananiandama hivi japo sikujua ni tatizo gani ambalo limenifanya niwepo nyumbani bahati nzuri ikaja akili ya mimi kutoa simu mfukoni na niwashe tochi ili hata nimulike lakini kabla cjawasha simu nasikia vicheko upande wa pili hapo ndipo ninapo changanyikiwa na kujihisi huenda labda linalotokea ni ndoto tuu na sio hali halisi, kwa kweli nilikuwa nimechanganyikiwa sio kidogo baada ya kama dakika kumi hivi umeme ukarudi na taa zote zikawashwa na kujikuta nipo mbele ya watu wanaonitazama tuu na kwa mbali nikasikia sauti ya Baba na Grace wakija huku wakiimba wimbo wa happybirthday,
"Happybirthday to you"
"happybirthday to you"
"happybirthday dear brother, happybirthday"
Nilijikuta kama damu sasa imeanza kurudi mwilini kwani muda mchache uliopita nilijihisi damu imehama njia na mwili kuachwa bila damu wala maji, kwa furaha nilyokuwa nayo kwa muda ule nikajikuta naanza kulia kwani ni lini mara ya mwisho nimefanyiwa party kama hii ninayoishuhudia mbele yangu nilikuwa nimesahau kwakweli, ni kitambo sana kwa kweli..
walisogea hadi nilipo mimi wakiwa na tololi la keki lililozungukwa na mishumaa kila kuna na baada ya kunikaribia nikakaribishwa kwa ajili ya kuizima mishumaa ile ili shughuli ianze rasmi, kwa furaha iliyoje nikalisogeza toroli karibu yangu kabla cjafanya chochote nikasikia sauti ikinitaka nisifany chochote
"aaaah jamani hamuwezi fanya hiyo kitu wakati mimi sipo wajameni"
"oooh jaman, Godlove" Grace aliongea hukui akimkimbilia kwa shangwe
"hahahahaha, yaani nilishajua huwezi kuja kwa sababu sherehe imechelewa kuanza kwa sababu yako ujue, tumekusubiri sana na ulinambia unawahi ndege ya kwanza" Baba nae aliongea kwa furaha huku wakikumbatiana kwa shangwe
"Aisee, yaani nimechelewa ndege zote huwezi amini dady, imenibidi nichukue private ambayo ndo ilikuwa imebaki pale store, lakini hakuna kilicho haribika kwani si nimefika mzee" aliongea huku akiwa ananikaribia na kunisalimia tukakumbatiana na kuendelea na matukio mengine
Binafsi nilikuwa sijui kinachoendelea kwani ndio mara ya kwanza namuona huyu kaka lakini anaonekana ni mjanja mjanja sana na ana uelewa wa kutosha na yuko smart sana, alikuwa amevalia t shrt nyeusi juu chini amevaa pensi kama niliyoyaa mimi, na baada ya kumwangalia vizuri niligundua kila alichovaa kilikuwa sawa na mimi, sikuelewa ni kwanini ila kwa sababu ilikuwa ni sherehe ya kunipongeza kuongeza mwaka mwingine sikujali sana kwani nitakuwa na muda wa kuuliza na kuambiwa yote nisiyoyajua..
"Lakini jaman hii siyo haki kabisaa yaan" aliongea Godlove
"Kwanini?" alihoji Grace
"Asa nyie mnataka mzimie mishumaa huku juu kwani kule chini hakuna watu?"
"Ila kweli hebu bwana sherehe tangulia kule gardeni kwanza wakati sisi tunakufuata nyuma,"
Na nikafanya kama walivyokusudiwa mi nikawa mbele wao wanakuja nyuma na torori la keki mpaka kufika gardeni nikakuta mazingira yamebadilika, pamepambwa vizuri kweli yaan na magari yaliyokuwa yamepakiwa hovyo yalipangwa vizuri, kwa kweli nilifurahi sana lakini nikawa najiuliza huyu kijana aliyekuwa anasubiriww amwanzo ni nani mpaka sherehe ichelewe kwa ajili yake na kingine kwann baba ameamua kufanya hii sherehe na sikuwahi fanyiwa miaka yote ambayo nilikuwa nao nije kufanyiwa leo, lakini yote kwa yote nilifurahi sana, kwani na mimi nilijiona ni mtoto wa pekee katika watoto ambao mzee mtweve alikuwa nao.
Baada ya kufika bustanini ndipo nikageuka na kuambiwa nizime mishumaa ambayo ilikuwa imeizunguka meza ya keki na nikafanya hivo huku nikisindikizwa na nyimbo pamoja na kelele za shangwe wakinishangiria kwa kufanikisha hatua hiyo huku na mimi binafsi nikijipigia makofi kwa furaha sana.. baada ya hapo ratibva zingine zikaendelea ilikuwa mida kama ya saa tatu hivi usiku ambapo ndio sherehe ilikuwa inaanza rasmi., wakati nmekaa na marafiki na badhi ya watu ambao nilikutana nao pale, wengine tulishawahi kukutana na baadhi walikuwa na sura ngeni machoni pangu, lakini wakati wote huu Godlove alikuwa karibu sana na mimi huku akinitambulisha kwa baADHi ya wafanya biashara na baadhi ya marafiki zake ambao alikuwa ameongozana nao kuja nao kutoka huko alikokuwa na baadhi nambao ambao aliwakuta hapahapa nchini.
"Jamani, ndugu jamaa na marafiki ambao mmefika maeneo haya kwa ajili ya shughuli hii muhimu ya kumpongeza kaka yangu kwa kuongeza mwaka mwingine naomba tusogee karinu na stage kuna kitu muhumi kaka anataka kuwafanyia, tafadhalini sana" Aliongea Grace kwa kutumia
kisemeo ni maneno yaliyonishtusha kidogo kuna nini ambacho wamekusudia nitakifanya, watu waliupokea ujumbe ule kwa makofi na kwa kelele nyingi, huku sielewi nitaenda kufanya nini pale jukwaani"Bwana mwenye maupendo yako, kaka mwenye maupendo yako kwa ndugu zako, bosi mwenye maupendo yako kwa wafanyakazi wako, mtoto mwenye maupendo yako kwa wazazi wako na kikubwa ni Mtanzania mwenye maupendo ya kutosha kwa nchi yako, nikiwa kama mtu muhimu kwako kama unavoniambiaga mdogo angu nakupenda nutafanya chochote kukufurahisha na leo nitaomba unifurahishe kaka yangu mpenzi, nikupendaye toka moyoni habay love" Aliendelea kuongea grace akiwa na furaha iliyokithiri kwa kweli
"nakuomba usogee jukwaani na upande pale juu pana mic"
Nikasogea pale juu na kuikuta mic kama nilivyoelekezwa..
"Unauona umati huu mbele yako?" aliongea Godlove huku wakiwa wamevalia mic zisizo za kushikilia
"Ndio nimeuona kaka,"
"sasa mimi na grace tumekurupuka tuu na kuja na wazo hili kama hutojali" aliongea huku akimshika mkono Grace na kunisogelea pale nilipokuwa nimesimama mimi.
"eenhe grace hivi tulipanga nini vile" aliuliza God akimtazama Grace kwa kutegemea majibu
"Anha, unajua nini?" aliongea Grace
"Hapana sijui labda unijuze wewe" alijibu God
"Baba ameishi kusema Kaka alikuwa na ndoto za kuwa mwimbaji na mwandishi wa insha"
"eenhe"
"sasa wakati wote baba ananiambia kwamba na wewe God unapenda sana kuandika simulizi, sasa nikiwa kama mdogo wenu mpendwa kila mmoja afanye kitu ambacho kitanifurahisha miomi lakini pia wageni waalikwa nao wafurahie uwepo wenu na mlivyovaa saresare naamini mtafanya kitu ambacho sote tutakifurahia au mnasemaje wageni waalikwa..."
"ndioooooo!!!" wageni waalikwa, ndugu jamaa na marafiki walijibu kwa furaha na mayowe baada ya kuyasikia maneno ya Grace.
Kiukweli ilikuwa suprise kwani kwani sikutegemea kabisa mimi kukutana na kauli kama aliyonambia Grace, lakini sikuwa na jinsi ilibid tu niperfom nyimbo ya Ed shareen shape of you, na God nae akaja kutupa simulizi nzuri kwelikweli iliyowaacha watu midomo wazi, basi baada ya hapo watu wote tulipata chakula cha pamoja na kama wasemavyo waswahili kuwa sherehe ni shibe ama kweli tulishiba, na baada ya hapo party ndo kwanza ikawa kama imechangamka kwani Grace aliposhika maiki na kutangaza kwamba sas tuparty mpaka ukafika muda watu wazima walienda kulala na kutuachia uwanja vijana na kucheza mziki na kuanza kucheza na kunywa... kwa kweli sherehe ilifana kweli yaani nilienjoy
"hey Habay mambo?" niliisikia sauti ya kike iliyojaa unyororo wa kutosha.
"pow habari yako" nilimjibu baada ya kunigusa begani
"am not good that way" alijibu kwa kingereza
"What do you mean?" nilimuuliza
"i just met with your brother, i think is just three weeks ago, so am not good at speaking swahili like u are" alinijibu tukijisogeza counter kuendelea kupata vinywaji
"ooh but still u can continues make it on your on with help of others who is round u and end of the day you will be good at that" nilimpa moyo kwamba aendelee kujifunza
"real?" aliniuliza kama ni kweli ninamaanisha kwa ninachokisema
"sure" nilimhakikishia kuwa ninamaanisha
"though i really like your talkative i would like to know it more than i am" aliniambia anapenda kujua zaidi kwani anakipenda kiswahili.
"you are welcome"
"thanks, and... i really like your performance ago" alisema, amefurahishwa na uimbaji wangu
"sure ?" nilimuuliza kama anamaanisha anachokisema
"yeah"
"thanks so much, and it was unprepared u know, she just came up with that i was bored due time but she is my young i can not denny it man and i just did for her happynes" yule ni mdogo angu hata kama alinishtukiza nilifanya ili kumfurahisha.
"u are good at that boe" ulifanya vizuri mbona
"ooh thanks dear" asante sana, nilimjibu huku nikitabasamu
"oky"
"eenhe, now tell me how they doing there?" nilimuuliza
"i think they are oky" alinijibu
"whaat, u think?"
"yeah i did not contact them for bit long you know, and i used to live in south africa" alinijibu yeye anaishi africa ya kusini hajawasiliana nao muda mrefu kidogo
" you are used to live in SA, and where are you from, homeland i mean" unaishi south africa na nyumbani ni wapi, nilimuuliza
"am from Somalia there they live my parents and i went SA for study and still i live there and met with Godlove there and we used to be friends verry close friends" ndio mi natokea Somalia ila nilienda Africa kusini kwa ajiri ya kusoma na nikawa nakaa kule na baadae kukutana na kaka ako.
"ooh thats why!!" aaah ndio maana
"whaat!! i dont get you, what do u mean?" niini sijakupata unamaanisha nn
"i used to hear that baes from somalia they are much beautiful and i did not got what they mean" nilikuwa nasikiaga tuu kama wanawake wa somalia ni wazuri na sikuwa naelewa wanamaanisha nini
"u have started ooh god"
"sure"
"oky, thanks even its not true" sawa hata kama sio kweli
"we will chart later, take this is my B.card, u know this party am the owner let get some things clear here" tutawasiliana namba yangu hii si unajua mi ndio mwenye sherehe hii
Basi baada ya kupiga stori mbili tatu mtoto wa kisomali niliendelea kuwasalimia wageni waalikwa na marafiki wengine ambao walihudhuria sherehe
"oooh habay, mambo vipi?"
"pow niambie" nilimjibu baada ya kumuona mtoto mzuri mweusi anaeng'aa kwa weusi wake asilia akinisalimia wakati huo pombe tayari ilishaanza kupanda kichwani
"fresh tuu vepe mtoto mdhuri?"
"safi tuu, kumbe unajua kuimba jamani" aliniuliza akitabasamu na tabasamu lake l lililojaaa uangavu na meno meupe mno mithili ya theruji
"aaah mbona kidogo tuu jaman" nilimjibu
"sasa habay..." aliniita akinishika mkono
"eenhe nambie mamaa" nilimjibu na mimi nikimshika vizuri mkono.
....ITAENDELEA...
0 Comments