Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Steve Nyerere sasa vita na Mwinyi Zahela

humph the GREAT
 Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahela
Msanii wa maigizo nchini, Steve Nyerere amesema kitendo cha aliyekuwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kwenda kwenye vyombo vya habari na kuzungumza kuhusu kufukuzwa kwake katika timu hiyo na anacho kifanya ni utoto, kwani wakati anatoa ile hela hakulazimishwa 

"Unajua yule mzee namshangaa sana zile habari za kutoka yeye na mguu wake kwenda na kusema mbele ya masikitiko yake kwamba uongozi wa yanga haumfanyii sahihi mimi naona kama ni mambo ya kitoto ambayo watu wazima kama sisi hata hatutakiwi kulizungumzia yaani mtu anatoa mchango wake kwa hiari yake mwenyewe halafu mwisho wa siku atataka kurejeshewa hapo naweza sema anataka kurejeshewa kwa sababu kama alikuwa na nia ya kuisaidia timu alitakiwa akae kimya na kama ana ugomvi au kumetokea na sintofahamu kati yake yeye na uongozi wa timu sio lazima sisi tujue kwamba yeye alitoa mchnago gani kwa timu wakati alitoa kwa moyo wake mwenyewe  labda kama uongozi walimuomba atoe mchango wake" alisema steve
 Mwigizaji na mchekeshaji Steve Nyerere

Post a Comment

0 Comments