Yanga yawatoa hofu mashabiki kutokuwa na chirwa

humph the GREAT

KIKOSI cha Yanga, kimeondoka jana asub­uhi kwenda Shelisheli kwa ajili ya mechi yake ya marudiano ya Ligi ya Mab­ingwa Afrika dhidi ya St Louis.

Hata hivyo, Yanga im­eondoka nchini bila kuwa na mshambuliaji wake wa kutumainiwa, Mzam­bia, Obrey Chirwa, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni majeruhi. Inadaiwa ana maumivu ya misuli.

Hata hivyo, Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, ame­watoa hofu wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwa, watashinda mechi hiyo hata bila ya kuwa na Chirwa.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Nsa­jigwa alisema kuwa wameji­panga kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi hiyo kwa hiyo anaamini kwa wachezaji walioondoka nao, wataiongoza timu hiyo kupata ushindi.

“Watu wengi walishitushwa na taarifa za Chirwa kutoku­wepo katika mechi yetu ya marudiano na St Louis, la­kini wanapaswa kujua kuwa mchezaji huyo siyo pekee ambaye hucheza uwanjani.



“Kwa hiyo, kuna mchezaji ambaye tumemwandaa ili kuziba nafasi hiyo na tunaamini atafanya vizuri, niwaombe tu wapenzi na mashabiki wetu kutokuwa na hofu na hilo, tutafanya vizuri,” alisema Nsajigwa.

Katika msafara wake huo, Yanga pia imewaacha Amissi Tambwe, Yohana Nko­mola, Donald Ngoma, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Thabani Kamusoko ambao ni majeruhi

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post