humph the GREAT
DAR ES SALAAM: MWANAMUZIKI
maarufu wa Bongo Fleva, Amini Mwinyimkuu ameamua kufunguka kuwa,
anatamani sana kuzaa na mwanamuziki mwenzake Esterlina Sanga ‘Linah’, ambaye kwa sasa ni mpenzi wake ambapo huko nyuma
walishawahi kuwa wapenzi wakamwagana kisha kurudiana. Akizungumza na
Ijumaa Wikienda, Amini alisema kuwa kama kuna kitu ambacho anakitamani
zaidi mwaka huu ni kumpachika mpenzi wake huyo mimba ili tu roho yake
itulie kitu ambacho anakiomba sana kwa Mungu, kitokee na anaamini kwa
mapenzi yake kitatimia.
“Hakuna mtu ambaye anajua kilichopo moyoni mwangu, nia yangu kubwa ni
kuzaa na Linah, napenda kuwa na mtoto naye si unajua kama mwanamke
unayempenda unatamani kuzaa naye ndio ilivyo kwa Linah, na Mungu
akipenda ni mwaka huu mambo yatakuwa mazuri,” alisema Amini ambaye leo
anatarajia kuachia video ya wimbo wao mpya waliofanya na Linah
unaokwenda kwa jina la Nimenasa.
Wawili hao kabla ya kurudiana hivi karibuni na penzi lao la sasa kuwa
motomoto, waliwahi kuachana miaka kadhaa iliyopita na kila mtu akashika
hamsini zake kwa kuwa na mtu mwingine. Baada ya kila mmoja kumwagana na
mtuwe kwa nyakati tofauti, wameamua kurejesha penzi lao kwa kasi na sasa
wamekuwa wakigandana kama ilivyokuwa zamani wakati penzi lao
linachipukia
0 Comments