Pigo jingine kwa MOI

humph the GREAT

 Rais mstaafu wa Kenya, Daniel Arap Moi ameamriwa na Mahakama Kuu jijini Nairobi amlipe fidia ya Ksh. bilioni 1.6 Susan Cheburet Chelungui na mwanawe David Chelungui kwa kosa la kutumia mamlaka yake vibaya na kuwanyang'anya shamba familia hiyo mnamo mwaka 1983

Mjane huyo aliporwa shamba lake kwa njia ya udanganyifu huku maafisa wakuu Serikalini wakitumiwa katika udanganyifu huo na kisha kuliuza shamba hilo kwa kampuni ya Rai Plywood (K) Limited

Mahakama ilisema kuwa mbali na Rais Moi, sehemu ya shamba hilo pia iligawiwa kwa aliyekuwa Waziri msaidizi kwenye utawala wa Moi, Stanley Metto

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post