Theresa May kujiuzulu kama kiongozi
wa chama cha Conservative tarehe 7 Juni na kutoa fursa kuidhinishwa
mchakato wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya Uingereza.
Katika
taarifa iliojaa hisia alioitoa huko Downing Street, Bi May amesema
amefanya "kila awezalo" kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya
mnamo 2016. Ni jambo linalosalia kuwa "na majuto mengi" kwamba
ameshindwa kutimiza Brexit - Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya,
ameongeza. Lakini waziri mkuu mpya ndio suluhu " kwa manufaa ya taifa"
Mpango wa Theresa May wa Uingereza
kujiondoa katika Umoja wa Ulaya umepingwa na wabunge kwa mara ya pili
huku zikiwa zimesalia siku 17 hadi muda wa taifa hilo kujitoa katika EU.
Wabunge
walipiga kura kupinga mpango wa waziri mkuu huyo kwa kura 149 -
kiwango kidogo ikilinganishwa na kura zilizopigwa Januari. Bi May
amesema wabunge sasa watapiga kura iwapo Uingereza iondoke katika EU
bila ya mpango na iwapo hatua hiyo itashindwa, kura ya iwapo mpango
mzima wa kujiondoa - Brexit uahirishwe. Waziri mkuu aliwasilisha
ombi la dakika ya mwisho kwa wabunge waunge mkono mpango wake baada ya
kupata hakikisho kisheria kuhusu msimamo wa Ireland kuhusu kujitoa
katika EU.
Mpango wa Bi May ni upi?
Akifafanua
mpango wake, amesema wabunge watarudi tena kupiga kura Jumatano kuhusu
iwapo Uingereza inastahili kuondoka EU na mpango au bila mpango. Iwapo
watapiga kura kupinga mpango , watapiga tena kura siku inayofuata
kuhusu iwapo kuidhinisha kurefushwa kwa kipengee cha Article 50 - mfumo
wa sheria utakao iondoa Uingereza katika EU kufikia Machi 29.
Bi
May amesema wabunge itabidi waamue iwapo wanataka kuahirisha Brexit,
kuandaa kura nyingine ya maoni au iwapo "wanataka kuondoka na mpango
lakini sio mpango ulioko".
Bi May amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati
kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama
cha Conservative. Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7
na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada
ya hatua hiyo.