humph the GREAT
Serikali
leo Juni 18, 2020 imeifungia timu ya JKT Tanzania kucheza bila
mashabiki katika michezo yake yote ya nyumbani ya Ligi Kuu msimu huu kwa
kosa la kutochukua tahadhari ya Kujikinga na corona katika mchezo wao
dhidi ya Yanga uliochezwa jana Jumatano katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma katika mchezo wao wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo imeeleza kuwa adhabu hiyo imeelekezwa kwa JKT Tanzania kwa
sababu wao ndio walikuwa timu mwenyeji.
“Katika mchezo huo na. 288 uliochezwa jana Jumatano, Juni 17, 2020,
mashabiki walijazana uwanjani na kukaa bila kuzingatia Kanuni ya 2.0.2
(iii) inayosisitiza kuachiana mita moja.
0 Comments