Facebook kuchochea ubaguzi

humph the GREAT
Kuna mengi utakayoyasikia katika matangazo yetu ya mchana ila haya ni baadhi tu. Tutafurahi ukitoa mchango wako kuhusiana na ripoti hizi mbalimbali;

✍Nchini Tanzania kunaonekana kuwepo kwa msukumo mpya ndani ya chama tawala CCM na hata  nje ya chama hicho kutaka Rais Samia Suluhu Hassan aungwe mkono  kuwania urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025. Lakini ni kwa nini hali hiyo inajitokeza wakati huu ambapo bado uchaguzi uko mbali?

▶Mwasisi na mmiliki wa kampuni ya Facebook, Mark Zuckerberg, amepinga vikali madai kwamba mtandao wake huo mkubwa wa kijamii unachochea migawanyiko na madhara yaliyotolewa jana na aliyekuwa meneja wake wa bidhaa, Frances Haugen, alipokuwa akitowa ushahidi mbele ya baraza la Seneti la Marekani.

🔦Wabunge wa bunge la Ulaya wanakutana mjini Strasbourg nchini Ufaransa, huku wakionyesha utayari wa kuishinikiza zaidi jumuiya ya kimataifa kumshitaki Rais wa Belarus Alexander Lukashenko anayehusishwa na ukandamizaji na mateso ya watu wengi. 

😷Wakimbizi katika mji wa Beni ulio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanalalamika kuwa watoto wao wanabaguliwa na viongozi wa baadhi ya shule mjini humo, wakati tayari muhula wa kwanza wa mwaka wa masomo ukiwa umeanza Jumatatu wiki hii. Wanasema hali hiyo haielweki wakati sera ya serikali ikiwa ni elimu ya msingi kwa watoto wote, tena bila malipo.

✍Rais wa Marekani Joe Biden amesema amezungumza na Rais wa China Xi Jinping kuhusu Taiwan na baada ya China kutuma idadi kubwa ya ndege za jeshi katika anga ya Taiwan.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post