Zari The Boss Lady
amefichua jambo ambalo wengi hawalijui kuwa, yeye ni mchanganyiko wa nusu Mhindi na nusu ni Msomali.
Zari
ambaye ni raia wa Uganda amekuwa mgumu mno kuzungumzia asili ya wazazi
wake. Mara chache aliwahi kuposti picha za mama yake, lakini hakuwahi
kumuelezea kiundani.
Wengi wanamfahamu Zari
kama mwanamke tajiri anayeishi nchini Afrika Kusini na ni mzazi mwenza
wa mwanamuziki wa Tanzania, Diamond Platnumz, lakini ukweli ni kwamba
ana simulizi nyingi kuhusu maisha yake hadi hapo alipo.
Lakini
hivi karibuni alifungua macho wafuasi wake zaidi ya milioni 9 kwenye
Instagram baada ya kuwatonya kuwa, wazazi wake ni mchanganyiko wa
Wahindi, watu wa Burundi na mchanganyiko wa Uganda na Somalia.
0 Comments