humph the GREAT
06.10.2021 Matangazo ya Asubuhi
-Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kamanda mpya wa kikosi maalumu cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa, jenerali Steven Mkande kutoka Tanzania ameshika wadhifa wake huo,wakati ambapo mikoa ya Kivu ya Kaskazini na Ituri iko katika hali ya dharura.
Wajumbe kutoka nchi 4 zinazo pakana na ziwa Tanganyika wanakutana mjini Bujumbura kujadili swala la mipaka ndani ya ziwa hilo iliowekwa tangu zama za ukoloni wa ujerumani.
-Shirika la UNICEF katika ripoti yake ya wiki hii, limetoa rai kwa serikali za dunia kuwa hazina budi kutenga fedha nyingi zaidi na rasilimali ili kusaidia kutunza afya ya akili ya watoto.
-Raia wa Afghanistan ambao wameikimbia nchi yao kuelekea Marekani wanakabiliwa na tatizo la shida ya makaazi.
-Nchini Ufaransa kumegundulika kiwango kikubwa zadidi cha unyanyasaji wa kingono 9kwa watoto katika Kanisa Katoliki.