Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Hasira za Manara Zamponza



1 Ukimuangalia MANARA jana alipokuwa ana hojiwa alionekana ni mtu mwenye uchungu sana mpaka alijisahau kabisa mpaka Diva mtangazaji alimuuliza upo na furaha kweli??


2 Mapenzi hayawezi kujificha MANARA SIMBA ndo club ya maisha yake kitendo kilichofanyika kumuondoa kimemfanya asifurahie tena mchezo wa mpira.


3 Jana amekili kama kuna kipindi alipata wakati mgumu ni kufanya maamuzi ya kuhamia YANGA lakini alifanya hivyo kwa ajili ya maisha tu ili familia iende na pia alijua kwenda YANGA simba itawauma sana hapa inaonekana alifanya maamuzi haya ili awaumize SIMBA ingawa leo anaonekana yeye ndo anaumia.


4 Swala la Fidia aliongelea kuhusu kwenda MAHAKAMANI kutaka kulipwa Fidia kwa kutumikishwa miaka sita bila mkataba lakini amesema anaandaa mawakili 10 nafikiri huwenda anajua ugumu wa madai anayoyadai ndo maana anaona kushindwa kwake kama hatajipanga.


5  Swala la kujipa mamlaka ya kwamba watanzania leo wengi wanapenda mpira kwa ajili yake hapa kidogo tunaomba awaombe radhi WATANZANIA  

MANARA amekaa SIMBA miaka sita na kabla ya hapo hakuna mtu alimjua MANARA ina maana kabla ya hii miaka sita watu walikuwa hawapendi mpira hawafuatilii mpira ni kweli ?


6 MANARA  anatakiwa kujua ya kwamba watu wameanza kuufuatilia huu mpira tangu baba yake anacheza mpira yeye akiwa bado hajazaliwa asipe mamlaka asiyokuwa nayo ni nani alimjua MANARA kabla ya kuanza kufanya kazi SIMBA? 


7 Swala la yeye kufanya jitihada ya kumshawishi Diamond ahamie YANGA yani hapa naona kama analeta utoto sana anasahau kuwa mapenzi ya wapenda soka yanatoka moyoni hata yeye wanasimba walimpenda sana sana ila inapofikia hatua ya mapenzi ya timu kama kweli wewe ni mtu wa soka huwezi kuhama timu kwa sababu yeyote ile na kama Diamond ataenda YANGA italeta maana kuwa hakuwa mtu wa mpira ni bendera fuata upepo.


8 Alilalamika kuwa viongozi wa SIMBA wanawalipa watu pesa eti wamtukane mitandaoni au wale watu wa YANGA wanaosema hawamtaki wamepangwa na SIMBA hapa anatafuta sehemu ya kujifichia anachotakiwa kukumbuka hawawezi watu wote wa YANGA wakakubali maneno yake kwa sababu wapo wanaoamini kuwa yupo YANGA kikazi na wao wanataka MWANAYANGA wa damu ndani ya timu yao.


9 Jambo baya alilolionesha jana ni kuonesha chuki ya wazi aliyonayo kwa Anthonio Ndugaz kwa kumuita Mnafiki na si mtu mkweli anajifanya mstaarabu kumbe hana lolote hapa niliumia sana sana ndugaz ni WANAYANGA kikwelikweli nilimshuhudia kigoma akiangusha chozi kwa ajili ya YANGA 


Hii laana ya kumuondoa  Ndugaz wana YANGA kwa ajili ya sababu za kibiashara hakika MUNGU hawezi kuwa upande wa YANGA Ndugaz ni binadamu na ana moyo yupo pembeni ila ipo siku atarudi YANGA ni jambo la muda tu


10 Ushauri MANARA kama kweli kaenda YANGA kwa moyo wake wote ifike mahala tumuone anaijenga YANGA kama alivyoijenga SIMBA jana kwenye kipindi hakuna hata sehemu moja ameongea kuhusu YANGA ameongea mgogoro wake tu wa nafsi ambao ule ni mgogoro wa kudumu


Safari ya MANARA ipo njiani pale WANAYANGA watakapoamua kuendesha timu kisayansi kama kuna watu wanamlea anatakiwa kukumbuka kuwa hao viongozi watapita watakuja wengine ni jambo la muda tu hawezi kushindana na Taasisi SIMBA ni dude kubwa lililobeba roho za watu wakiwemo viongozi wakubwa wa nchi wanaomtuma wamuwekee mipaka kama wanampenda kweli.

Post a Comment

0 Comments