Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

ulizozikosa kwenye michezo

Tetesi za Soka Ulaya Mbappe, Pogba, Tchouameni, Sterling, Lewandowski, Rice

Kylian Mbappe in action for PSG

CHANZO CHA PICHA,EPA

Maelezo ya picha,

Kylian Mbappe alijiunga na PSG mwaka 2017 katika uhamisho wa thamani ya £165.7m

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, hatasaini mkataba mpya Paris St-Germain haijalishi klabu hiyo ya Ligue 1 itamlipa kiwango gani cha fedha kwani nyota huyo ameamua kuelekea Real Madrid. (AS - in Spanish)

Liverpool, Manchester City na Manchester United awanamnyatia kiungo wa kati wa Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 21, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa karibu £40m. (ESPN)

Manchester City wanapanga kujaza pengo litakaloachwa na mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 26, na mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33. (Express)

Robert Lewandowski

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Manchester City wanamtaka Robert Lewandowski kuchukua nafasi ya Raheem Sterling

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekubali kuwa kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 28, huenda asishawishike kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo mpaka apatiwe muda zaidi wa kucheza. (Evening Standard)

Wakala wa Paul Pogba, Mino Raiola amemtoa kiungo huyo wa kati wa Manchester United kwa Barcelona. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa wa miaka 28- katika uga wa Old Trafford unatarajiwa kumalizika msimu ujao na Raiola amewasiliana na Juventus, Paris St-Germain, Real Madrid klabu zingine kadhaa za Ligi ya Primia. (ESPN)

Paul Pogba

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Wakala wa Pogba amewasiliana na Juventus, Paris St-Germain, Real Madrid klabu zingine kadhaa za Ligi ya Primia

Mshambuliaji wa Everton na England Dominic Calvert-Lewin, 24, ni chaguo la kwanza la Arsenal msimu ujao. (Football.London)

Mkufunzi wa Roma Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Riqui Puig, 22, ambaye amepoteza umuhimu kwa safu ya ukufunzi huko Nou Camp. (Sport - in Spanish)

Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger "ameghadhabishwa" na ofa ya Chelsea ya hivi karibuni. Mkataba wa sasa wa nyota huyo wa miaka 28-unamalizika mwisho wa msimu huu. (Sport1 - in German)

Toni Rudiger

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger

Kocha wa zamani wa Shakhtar Donetsk na Roma Paulo Fonseca ameibuka tena na anapigiwa upato kujiunga na Newcastle, ambayo inatarajiwa kumtimua Steve Bruce ndani ya wiki chache zijazo. (ESPN)

Wakilishi wa Declan Rice, 22, wamepuuzilia mbali tetesi zinazomhusisha na kiungo huyo wa kati wa West Ham na England na uhamisho wa Newcastle. (90Min)

Inter Milan wana matumaini ya kumshawishi kiungo wa kati wa Italia Nicolo Barella, 24, kusaini mkataba mpya ijapokua ananyatiwa na Liverpool na PSG. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Declan Rice

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Wakilishi wa Declan Rice, 22, wamepuuzilia mbali tetesi zinazomhusisha na Newcastle

Eintracht Frankfurt hawatarajii winga wa Serbia Filip Kostic, 28, atajiunga na Newcastle mwizi Januari mwakani. (Sport1 - in German)

Beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher anasema pesa sio dhamana ya kufanikiwa na atashangaa Newcastle ikichukua taji la Ligi Kuu kabla ya 2030. (Telegraph - subscription required)

Kiungo wa kati wa Rangers Joe Aribo, 25, ananyatiwa na Crystal Palace. (Football Insider

Post a Comment

0 Comments