Picha za Helikopta iliyopata ajali ikiwa imembeba Makamu wa Rais na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania "Gharib Bilal" , Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam "Said Meck Sadick" pamoja na kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam "Suleiman Kova" hapo jana walipata ajali na Helikopta waliyokuwa wamepanda asubuhi ya jana (April 13 2014) wakati wanaruka kutoka kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam .
Ajali hii imetokea wakati viongozi hawa wakiruka na helikopta hiyo kuelekea kwenye maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua zinazoendelea kunyesha jijini dar es salaam.
Viongozi hawa walinusurika kifo kwenye ajali hiyo lakini wamepata majeraha madogomadogo. Tunawapa pole sana kwa ajali iliyowapata
Tags
News



