KIFO cha msanii wa filamu, Rachel Haule kimewaumiza wengi lakini baadhi yao ni wasanii wenzake, Halima Yahaya ‘Davina’ aliyeachiwa hausigeli wa marehemu katika mazingira ya ajabu huku Wastara Juma akiumizwa na viatu na pochi alivyopewa na Rachel kabla hajafariki dunia.
Akizungumza na Ijumaa juzi, Davina alisema alihangaika sana kumtafutia Rachel hausigeli ili atakapojifungua asipate shida lakini siku moja kabla ya kifo, alipompigia simu akitaka ampelekee mtu wake simu haikupokelewa hadi alipopata taarifa za kifo.
“Aliniambia nimtafutie msichana, nikafanya hivyo, wakati najipanga kumpelekea nyumbani kwake nasikie eti kafariki, naumia sana,” alisema Davina.
Tags
Bongo movie