Neno! Staa
wa sinema za Kibongo, Wastara Juma, bila kumung’unya maneno amefunguka
kwamba kufuatia mfarakano ndani ya Klabu ya Bongo Movie Unity hadi
kufikia hatua ya aliyekuwa mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’ kujiuzulu, kumewachafua kwa viongozi serikalini hasa Rais Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda,
wikiendi iliyopita jijini Dar, Wastara alisema anawashangaa wasanii
wenzake wanaoendekeza majungu kutokana na wivu wa maendeleo na
kusababisha klabu hiyo kutosonga mbele badala na kuonekana kituko.Wastara alisema kuwa jambo hilo lisiporekebishika hali haitakuwa shwari klabuni hapo hata kama atachaguliwa mwenyekiti mwingine.
Tags
Bongo movie