MTANGAZAJI MAIMARTHA JESSE AMLIZA DAVINA WA BONGO MOVIE


Ni shida! Mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’, hivi karibuni alimliza staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ baada ya kuchelewa kufika ukumbini akiwa MC (Master of Ceremony) kwenye shughuli ya mdogo wake (Davina)
Mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’.
Mpango mzima ulijiri wiki iliyopita nyumbani kwa Davina maeneo ya Mbezi Beach, Dar ambapo staa huyo alijikuta akihaha hadi alipojitokeza Eva wa Dude na kulianzisha.
Hata hivyo, nusu saa baadaye, Mai alitimba huku akimsindikiza bi harusi na kujitetea kuwa gari lake lilipata pancha barabarani.
Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’.
Baada ya Mai kuingia, Eva alimkabidhi ‘maiki’ kisha shughuli ikaendelea lakini baadaye ilionekana kuwa mkosi kwa Mai kwani shughuli ilipoisha, alilalamika kuibiwa redio ya gari lake ingawa haikujulikana kama iliibwa mahali hapo au alipopata pancha.
Pamoja na yote, shughuli ilipendeza na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa mjini.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post