humphrey the GREAT
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa
Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Newcastle Bwana Paul Jeans Chuoni hapo nchini Australia jana tarehe
29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kutunukiwa shahada ya heshima
ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia.
Sehemu ya umati wa wanachuo na wageni waalikwaa waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada hiyo.
Sehemu ya Watanzania waishio nchini Australia wakipiga makofi wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitutunukiwa shahada hiyo.
Rais
Kikwete akimpongeza Bi. Bernadette Mathias ambaye kwa kushirikiana na
mpiga piano mumewe Profesa Philip Mathias walitumbuiza kwa wimbo wa
“Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote” kwa ufasaha na kusisimua
waliohudhuria sherehe hizo.
Rais
Kikwete na msafara wa wanachuo wakiondoka jukwaa kuu huku
wakishangiliwa na waliohudhuria ikiwa ni pamoja na Mama Salma Kikwete na
mwana wao Ali Kikwete na ujumbe wa Rais Kikwete kwenye msafara huo.
Mama
Salma Kikwete akimpongeza mume wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa
kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws
honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle.
Rais
Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Newcastle
na mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa
shahada.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Ujumbe alioongozana nao mkewe
Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
Rais
Kikwete katika picha ya pamoja mkewe Mama Salma kikwete, mwana wao Ali
Kikwete na Watanzania waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada.
Rais Kikwete akipongezwa na raia wa Burundi waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada.
Tags
kikwete