humph the GREAT
MWANAMUZIKI mwenye jina kubwa
Afrika, 2 Face Idebia amempa shavu la mwaliko diva anayekimbiza kwenye
Tasnia ya Muziki Bongo, Vanessa Mdee ‘V Money’ kwenye tamasha lake
litakalofanyika leo jijini Nairobi, Kenya huku wasanii mbalimbali kutoka
kila kona ya Afrika wakitarajia kufanya makamuziki ya ukweli.
Akizungumza na gazeti hili, V-Money
anayetamba na Wimbo wa Niroge kwa sasa amesema shavu hilo kwake ni kitu
kizuri maana kimeonesha ni jinsi gani wasanii wa nje wanavyothamini kazi
zake hata kuamua kumpa mwaliko ambao mbali na kutangaza ngoma yake ya
Niroge atapata fursa ya kukutana na wasanii wengi ambao anaweza kupata
wa kufanya nao kazi.
“Namshukuru Mungu kazi zangu
zinaheshimika, mwaliko wa 2 Face ni muhimu kwangu na nimeuchukulia kwa
uzito kutokana na tamasha lenyewe litakavyokuwa kubwa, nina uhakika
sitaondoka bure, lazima nitapata lolote la kufanya kwa mashabiki wangu,”
alisema V- Money.
Tags
wasanii