humph the GREAT
Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, ACP Martin Otieno
Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, ACP Martin Otieno
UWAZI
DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es
Salaam limemnasa raia wa Nigeria, aliyetambulika kwa jina la Dede Eke
(45) baada ya kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroine kilo
tano uwanjani hapo.
Akizungumza na Uwazi, ofisini kwake
Ijumaa iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, ACP
Martin Otieno (pichani) alithibitisha kukamatwa kwa Mnigeria huyo siku
hiyo akasema kulitokana na kuimarisha ulinzi uwanjani hapo na kufungwa
mashine za kisasa za uchunguzi.
“Ni kweli tumemkamata Mnigeria Bede Eke
katika Uwanja wa Ndege Dar na kilo tano za dawa za kulevya aina ya
heroine wakati akitaka kuondoka kwenda Lagos, Nigeria kwa ndege. Dawa
hizo zimepelekwa kwa mkemia mkuu kwa uchunguzi na kujua thamani yake.
“Dede alikuwa ameficha madawa hayo
katika begi dogo jeusi ambalo alishonea madawa ndani kisha
akalitumbukiza ndani ya begi kubwa, amenishangaza, alidhani hatupo
makini!” alisema kamanda huyo na kuongeza kuwa polisi wanamhoji
mtuhumiwa huyo kujua alikozipata na upelelezi ukikamilika tutamfikisha
mahakamani.
Tags
HABARI