humph the GREAT

HATIMAYE ile safari ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba iliyoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, jana Alhamisi ilifika tamati baada ya kudumu kwa takribani miezi sita, ambapo kulifanyika kwa droo kubwa katika Viwanja wa Zakhem, Mbagala jijini Dar na mshindi kupatikana.
Nelly Mwangosi mkazi wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni mama wa nyumbani mwenye watoto wawili ndiye aliibuka mshindi wa nyumba hiyo ya kisasa iliyopo Salasala jijini Dar yenye samani zote za ndani mpya kabisa na mshindi huyo anatarajia kukabidhiwa mali yake hivi karibuni.

Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo akisoma jina la mshindi wa nyumba, ambaye ni Nelly Mwangosi kutoka Iringa.
MC Chaku akimpigia simu mshindi wa nyumba, Nelly Mwangosi kutoka Iringa.
Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo akizibwa macho ili akachague kuponi ya mshindi.
Abdallah Chaurembo akiwa na kuponi ya mshindi wa nyumba.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akiwashukuru Watanzania wote walioshiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.
HATIMAYE ile safari ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba iliyoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, jana Alhamisi ilifika tamati baada ya kudumu kwa takribani miezi sita, ambapo kulifanyika kwa droo kubwa katika Viwanja wa Zakhem, Mbagala jijini Dar na mshindi kupatikana.
Nelly Mwangosi mkazi wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni mama wa nyumbani mwenye watoto wawili ndiye aliibuka mshindi wa nyumba hiyo ya kisasa iliyopo Salasala jijini Dar yenye samani zote za ndani mpya kabisa na mshindi huyo anatarajia kukabidhiwa mali yake hivi karibuni.
Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers, Oscar Ndauka akichukua zawadi ya Dinner Set tayari kumkabidhi mshindi.
Mara baada ya kupigiwa simu kutaarifiwa
kuwa yeye ndiye mshindi, mama huyo alisema “Yesu wangu!! Nimefurahi
kuona kuwa nimeibuka mshindi, najisikia raha sana, nawaombea Global kwa
Mwenyezi Mungu.” Shughuli hiyo ilitarajiwa kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye hata hivyo aliwakilishwa na Meya
wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo ambaye ndiye aliyesoma jina la
mshindi huyo.
Bahati nasibu hiyo ya Shinda Nyumba ilisimamiwa na Afisa Mwandamizi
wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo akimkabidhi Peter Mihayo zawadi ya Bedsheet.
Mbali na mshindi wa nyumba, pia kulikuwa na
zawadi ndogondogo zilizotolewa kwa washindi wengine. Washindi hao ni
Peter Mihayo, Issa Leon Mallya, Frank Ndambo (wote Bed sheets), Mahmoud
Mhina alishinda vyombo vya nyumbani (Dinner set) huku Method Kunambi na
Halima wakishinda simu ya kisasa (Smartphone).

Mahmoud Mhina akitokomea na zawadi yake ya Dinner Set.
Wengine ni ving’amuzi vitano vya TING
ambapo washindi wake ni Godfrey Mkombo wa Morogoro, Wilbert John mkazi
wa Kinondoni, Dar, Baltazar Mrosso kutoka Moshi, Magreth Ndambo wa
Tabata, Dar sambamba na Jane Liwinga mkazi wa Dodoma. Pia Hawa Maulidi
mkazi wa Mlole, Kigoma alishinda Bed Sheet, huku Helman Haule wa Dodoma
akijinyakulia Dinner Set.
Mmoja wa Ma MC wa kilele cha bahati
nasibu ya Shinda Nyumba, Kelvin Shayo (kushoto) akiwa na mmoja wa
wasomaji wa magazeti ya Global aliyekuwa akisoma jina la mshindi wa
zawadi ya Bedsheet.
Bahati nasibu hiyo ya Shinda Nyumba ilikuwa
ikiendeshwa na kampuni hii kupitia kwa magazeti yake ya Risasi, Amani,
Uwazi, Championi, Ijumaa Wikienda yanayopatikana kwa shilingi 500 huku
lile la Ijumaa linalotoka Ijumaa likiuzwa kwa shilingi 1,000 pekee.
Burudani wakati wa kilele cha bahati nasibu ya Shinda Nyumba.
Wakati mchakato wa kuelekea kumpata mshindi
huyo jana ukiendelea, wananchi wengi walionekana kufurahishwa na
kilichokuwa kikitokea huku wakisema kuwa Global imeweka historia kwa
kuwa tukio kama hilo ni nadra kutokea kwa shilingi 500 kumpatia nyumba
mtu tena ndani ya Dar es Salaam.

Mshindi wa simu ya kisasa (Smartphone), Method Kunambi (kulia) akipokea zawadi yake.
Aidha, kuna wale ambao walionekana kuwa na
furaha kupitiliza na kujikuta wakitoa machozi ya furaha kwa kuona nyumba
hiyo imeenda kwa mama wa nyumbani ambaye hana kazi. Katika maelezo yake
Nelly alisema kwa sasa ana watoto wawili lakini alikuwa nao wanne,
wawili walishatangulia mbele ya haki.
Zoezi la kusoma majina ya washindi wa zawadi ndogondogo likiendelea.
Tags
Burudani