humph the GREAT
Msanii Alikiba amefunguka na kusema kuwa yeye katika muziki wake hakuna mtu anayeshindana naye na kudai ila kama kuna watu wanataka kushindana na yeye basi atawaacha na kuendelea na mambo yake.
Msanii Alikiba
Msanii Alikiba amefunguka na kusema kuwa yeye katika muziki wake hakuna mtu anayeshindana naye na kudai ila kama kuna watu wanataka kushindana na yeye basi atawaacha na kuendelea na mambo yake.
Msanii Alikiba
Alikiba
anasema katika maisha yake ya muziki hataki kuona mtu yoyote anamtoa
katika njia yake, ndiyo maana watu ambao wanakuwa wakiongea ongea sana
juu yake yeye na muziki wake hawapi nafasi, kwani anaamini akiwapa
nafasi wanaweza kumtoa kwenye mambo ambayo yeye amekusudia kuyafanya
hasa zaidi katika muziki wake.
Mbali na hilo Alikiba amesema yeye haangalii ushindani na wala hashindani na mtu
"Unajua kila binadamu ana
tabia yake, kuna wengine wanajua kabisa kwamba wanakosea lakini
wanafanya hivyo kwa sababu na wapo wengine wanakuwa wanaongea
pasipokujua kama wanakosea, hivyo mimi kama msanii sitakiwi kusikiliza
hivyo vitu sababu nakuwa na mipango na malengo yangu, hivyo sitaki mtu
yoyote aniingilie kwenye mipango yangu kwa hiyo ukiwafuata unaweza
kujiangusha" alisema Alikiba
"Mimi siangalii ushindani na
wala sishindani na mtu ila kama wapo wanashindana na mimi nitawaacha
washindane na mimi lakini mimi sishindani ila naangalia malengo yangu na
mipango yangu katika muziki" alimalizia Alikiba