Msanii Dully Skyes ambaye sasa
anafanya vyema na ngoma yake 'Yono' amefunguka na kusema kuwa yeye
alianza kufanya muziki wa bongo fleva ili awe mtu maarufu na kuanza
kupata wanawake.
Msanii Dully Skyes
Dully
Skyes alisema hayo leo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Planet
bongo ya East Africa Radio kwenye Heshima ya bongo fleva na kusema miaka
kumi na kitu iliyopita aliamua kuingia kwenye muziki na kuwa msanii ili
apate wanawake.
"Mimi niliamua kuwa msanii
ili kwanza niwe maarufu nipate mademu tu na kupendwa na wasichana kwa
hiyo wala sikufikiri kuwa msanii ili nipate pesa ndiyo maana hata
nilipolipwa elfu mbili kwa ajili ya show nilikubali japo nilitakiwa
kulipwa elfu tano, tena hiyo elfu mbili niliona nyingi na nikamlipa
Queen Darleen mia tano sababu nilikwenda naye kwenye show. Kwa hiyo
sikuwahi kufikiria kama muziki ungekuwa biashara kama ilivyo sasa, saizi
nafanya muziki biashara ikitokea hao wanawake wametokea ni 'by the way'
tu" alisisitiza Dully Skyes
Dully Skyes ni moja kati ya wasanii ambao atakuwepo kwenye tamasha la
'Heshima ya bongo' fleva ambalo litafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe
1/7/2017 katika ukumbi wa Dar Live Mbagala ambapo wasanii wengine kama
TID, Dudubaya, Juma Nature, Z Anto, Solid Ground Family, Mabaga Fresh,
Mandojo na Domokaya na wasanii wengine watawasha moto kwa ngoma zao kali
za zamani.
0 Comments