Msanii Ben Pol amefunguka ya moyoni baada ya kukutana kwa mara ya
kwanza na mchekeshaji Ebitoke kwa kusema anaamini watu wengi wameoa ama
kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu ya kushindwa kuelezea hisia zao.
Ben
amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya mchekeshaji
Ebitoke kuonesha hisia za mapenzi katika mitandao ya kijamii kwa
takribani majuma mawili hivi sasa.
"Hakuna kitu kizuri kama
kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona kuna jambo zuri la
kujifunza, ikiwa unampenda mtu au unatamani nafasi fulani, utajuaje kama
unaweza kuipata hiyo nafasi au la ikiwa haujaiomba kwa muhusika ?.
Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa
sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale wawapendao.
Mwishowe walipokuwa tayari kuwaambia ikawa 'too late" aliandika Ben Pol.
Pamoja na hayo, Ben aliendelea kusema
"Ikumbukwe humu duniani sisi sote tunapita na labda huyo mtu kesho
hatokuwepo. Ebitoke umenifundisha jambo kubwa sana maishani, najua wengi
walikubeza sana wengine walikuambia hautaweza hata kuonana na mimi
laini huwezi amini mimi nimefurahi mno, kukutana na wewe na kuongea" alisisiza Ben Pol
Kwa upande mwingine Ben amesema amepata
jambo kubwa sana kupitia Ebitoke na kuahidi kuyaishi maneno yake siku
zote mwa maisha yake. https://youtu.be/bcScPRMkOd0?t=323